RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Kazi Misungwi District Council August 2024

Filed in Ajira by on 09/08/2024

NAFASI za Kazi Misungwi District Council August 2024

NAFASI za Kazi Misungwi District Council August 2024

NAFASI za Kazi Misungwi District Council August 2024

NAFASI za Kazi Misungwi District Council August 2024, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi anapenda kuwatangazia Watanzania Wote kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia barua yake yenye Kumb Na. FA.170/359/01B/89 ya tarehe 31 Mei,2024 na barua yenye Kumb Na.FA.97/288/01/09 ya terehe 25 Juni,2024 zimetoa idhini ya kutangaza na kuajiri nafasi za kazi za Masharti ya kudumu kwa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi zilizoidhinishwa kupitia Bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024.

Hivyo, Watanzania wote wenye sifa mnaruhusiwa kuomba nafasi hizo kama ifuatavyo:-

✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III (VILLAGE EXECUTIVE OFFICER III)- NAFASI KUMI NA MBILI (12)

MAJUKUMU YA KAZI

  • Afisa Masuuli na mtendaji mkuu wa serikali ya kijiji;
  • Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji;
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji;
  • Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri yakijiji;
  • Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
  • Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
  • Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaaluma katika kijiji;
  • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji;
  • Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji;
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
  • Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za kijiji; na
  • Atawajibika kwa Mtendaji Mkuu wa Kata.
  • Pamoja na kazi nyingine utakazopangiwa na Mwajiri wako

SIFA ZA MUOMBAJI
Waombaji wanatakiwa wawe wenye Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form Six) aliyehitimu astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

MASHARTI YA KAZI; Ajira ya Kudumu (Permanent Terms)

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B1.

✅DEREVA DARAJA LA II (DRIVER II) -NAFASI (02).

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kukagua gari kabla ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari. Kufanya usafi wa gari.
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.

SIFA ZA MUOMBAJI.

  • Awe Mtanzania mwenye umri kuanzia 18-45.
  • Awe amehitimu na kufaulu Kidato cha IV au VI.
  • Awe na Leseni ya Dereva daraja la E au C1 ya uendeshaji magari ambayo ameifanyia kazi kwa muda usiopungua miaka miwili bila kusababisha ajali.
  • Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha mafunzo (VETA) au chuo kingine kinachotambuliwa na serikali.

MASHARTI YA KAZI: Ajira ya Kudumu (Permanent Terms).

NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya Mshahara ni TGS B1 kwa mwezi.

MASHARTI YA JUMLA (MUHIMU YAZINGATIWE).

  • Maombi yote yatumwe na nakala za vyeti vya taaluma na cheti cha kuzaliwa, nakala za vyeti vithibitishwe na mahakama au mwanasheria aliyeidhinishwa au kutambulika na serikali.
  • Testmonials’ Provisinals Results’, Statement of Results, Hati za matokeo ya kidato cha nne na sita HAVITAKUBALIWA.
  • Maombi yaambatane na nakala ya kitambulisho cha Utaifa au namba ya kitambulisho cha Taifa.
  • Waombaji waliosoma nje ya nchi ya Tanzania wahakikishe kuwa vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika ya NACTE, NECTA au TCU.
  • Watumishi wote waliowahi kufanya kazi katika utumishi wa umma wakaacha kazi, kustaafu, wakastaafishwa, kufukuzwa kazi hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Utumishi.
  • Vyeti vyote vitafanyiwa uhakiki kwa kushirikiana na mamlaka husika NECTA na TCU.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
  • Mwombaji aambatishe picha mbili za rangi (passport size) za hivi karibuni. Maombi yaambatishwe na maelezo binafsi (CV).

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15.08.2024 saa 9:30 Mchana.

DONWLOAD PDF HAPA

Tags:

Comments are closed.