NAFASI za Kazi RUWASA August 2024
NAFASI za Kazi RUWASA August 2024
NAFASI za Kazi RUWASA August 2024, Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya
Karatu kwa niaba ya vyombo vya utoaji huduma ya maji ngazi ya jamii
(CBWSOs) vya JUWAMAKIHU, BAEWASU, ENDAWASU, BASHAWASU, GYEWASU, ENDAMIKO, MANG’OIA BARAZANI, IAGHANGARER NA MALECKCHAND anatangaza nafasi za kazi za wasimamizi (Fundi wakuu) na Afisa hesabu/ mtunza fedha wa vyombo vya utoaji huduma za maji ngazi ya jamii (CBUUSO, tajwa hapo juu kama ifuatavyo:-
WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI
✅FUNDI MKUU/MSIMAMIZI WA MRADI (SUPERVISOR)- NAFASI 8
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe mtanzania mwenye akili timamu na anyejua kusoma na kuandika.
- Awe na elimu ya kidato cha nne au zaidi.
- Awe na cheti cha ufundi stadi Maji daraja la tatu (Irade Test 6rade
lll/CBET Level l) au zaidi. - Awe na uzoefu wa kufanya shughuli za ufundi katika miradi ya Maji kwa
kipindi kisichopungua mwaka 1. - Awe na umri kuanzia miaka l8 hadi 45.
- Awe na uwezo wakutumia kompyuta (word, excel, internet, accounting software’s etc.),
- Awe ni mtu muadilifu na mwaminifu na ambaye hajawahi kushtakiwa kwa tuhuma zozote.
- Awe na uwezo wa kufanya kazi pasipo kusimamiwa pamoja na uwezo wa kuwasimamia watumishi waliochini yake.
- Wasimamizi wa vyombo ya utoaji huduma ya maji ngazi ya jamii
MANG’OLA BARAZANI, GYEIUASU NA ENDAIOUAU wawe NA Chcti ChA Diploma ya ufundi bomba kutoka chuo cha maji au chuo chochote kinachotambulika na Serikali.
Majukumu ya Fundi Mkuu/Msimamizi wa Mradi (Supervisor)
- Atafanya kazi chini ya kamati ya chombo (Community Water Committee).
- Atakuwa ndiye msimamizi na mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za chombo.
- Atakuwa ndiye katibu wa chombo na katibu wa vikao na mikutano yote ya chombo.
- Ataandaa na kusimamia
yote ya chombo. - utaratibu wa maandalizi ya vikao na mikutano
- Atakuwa na jukumu la kusimamia utoaji wa huduma bora ya maji kwa wateja wote.
- Kusimamia matengenezo yote ya miundombinu ya maji na kuhakikisha kuwa huduma ya maji inapatikana kwa wakati.
- Kuandaa taarifa zote za usimamizi, uendeshaji na matengezo ya mradi wa maji za kila mwezi, kila baada ya miezi matatu, kila nusu mwaka na taarifa za mwaka na kuwasilisha katika kikao cha kamati ya maji ya chombo.
- Kuaandaa na kusimamia utekelezaji wa bajeti ya mradi na huduma ya maji na kusimamia mapato yote na matumiziya chombo cha huduma ya maji.
- Kuhamasisha uchangiaji wa huduma ya maji na kutatua ama kutoa suluhisho la migogoro yote baina ya wateja na chombox. Kusimamia manunuzi ya vifaa vya mradi na huduma ya maji kwa kufuata taratibu zote za manununzi.
✅AFISA HESABU/ MTUNZA FEDHA- (MSIMAMIZIWA HESABU ZA CHOMBO) – NAFASI 5
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe mtanzania mwenye akili timamu na anyejua kusoma na kuandika.
- Awe na elimu ya kuanzia kidato cha nne na kuendelea
- Awe na cheti cha uhasibu daraja la tatu au zaidi
- Awe na umri usiopungua miaka 18 hadi miaka 45
- Awe na uwezo wakutumia kompyuta (word, excel, internet, accounting software’s etc.),
- Awe ni mtu muaminifu na mwadilifu na ambaye hajawahi kupatikana na hatia ya kosa lolote
Majukumu ya Afisa hesabu/ mtunza fedha
- Atafanya kazi chini ya Fundi Mkuu/Msimamizi wa Mradi (Supervisor).
- Atakuwa ndiye msimamizi wa mausuala yote ya fedha katika chombo
- Atasimamia na kupokea malipo ya maji na michango mbalimbali kwa
kuzingatia taratibu zote za makushanyo ya fedha - Ataandaa taarifa ya mapato na matumizi na kuiwasilisha kwa Fundi Mkuu/Msimamizi wa Mradi (Supervisor) kila mwezi, miezi mitatu, miezi sita na mwaka pamoja na kuziwasilisha katika vikao vya Chombo cha
Utoaji Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii na ofisi ya RUWASA Wilaya. - Kutunza vitabu vya fedha, hati za malipo mbalimbali na nyaraka zote za uthibitisho wa malipo mbalimbali/matumizi ya fedha ikiwa ni pamoja na kuandaa na kutunza kubukumbu/nyaraka zote za fedha
- Atafanya malipo baada ya kuidhinishwa na Fundi Mkuu/Msimamizi wa Mradi (Supervisor)
- Kushirikiana na Fundi Mkuu/Msimamizi wa Mradi (Supervisor) katika maandalizi ya bajeti ya mradi na kusimamia utekelezaji wa bajetibPamoja na majukumu mengine atakayopangiwa na Chombo cha Utoaji Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii na ofisi ya RUWASA Wilaya.
MASHARTI YA KAZI NA MSHAHARA
- Ajira zote tajwa hapo juu ni za mkataba ya miaka mitatu (3) na miezi sita ya mwanzo ni muda wa matazamio kabla ya kupewa mkataba.
- Mwombaji atakayefanikiwa kuajiriwa atalipwa mshahara kulingana na makusanyo pamoja na viwango vya mshahara viliyowekwa na chombo cha Utoaji Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii husika.
- Mwombaji awe tayari kufanya kazi katika eneo lolote atakalopangiwa na mwajiri wake.
MAELEZO YA JUMIA KIUA UUAOMBAJI WOTE
- waombaji wote waandike barua za maombi kwa mkono.
- Kwa wale waliosoma nje ya nchi ya Tanzania wahakikishe vyeti
vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika ffCU na NECTA) kulingana na ngazi
Ya cheti. - Maombi ya nafasi zakazi
yawe na viambatisho vifuatavyo:-
a) Wasifu binafsi (CV) yenye anuani za wadhamini wawili zikiwa na
mawasiliano kamili (mdhamini awe na barua ya utambulisho kutoka
kwa mtendaji wa mtaa/Kijiji anachokaa
b) Nakala za vyeti mbalimbali vya taaluma (Kitado cha nne, sita. chuo cha ufundi, ujuzi, cheti cha kuzaliwa na kitambulisho
cha Taifa/Namba ya NIDA) vilivyothibitishwa na mwanasheria/wakili.
c) Picha ndogo (passport size) moja (l) iliyopigwa hivi karibuni
Mwombaji mwenye sifa anatakiwa kutuma maombi kupitia posta au kupeleka ofisi ya RUWASA (W) Karatu kwa anuani ifuatayo;
Meneja wa RUWASA (W)’
s.L.P 203,
NMC-Karakana Ya Halmashauri,
Karatu.
Maombi ya kazi yanawezwa kutumwa kwa barua pepe [email protected]
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 14/08/2024 saa 9:30 alasiri’
maombi yote yatakayowasilishwa baada ya muda huo HAYATAPOKELEWA’
MUHIMU:
- Maombi ya wakazi wa maeneo ya miradi yatapewa kipaumbele,
- Wanawake wanahamasishwa kuomba nafasi hizi’