NAFASI za Kazi Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi August 14-2024
NAFASI za Kazi Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi August 14-2024
NAFASI za Kazi Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi August 14-2024,Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) inatarajia kufanya zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Tanzania Zanzibar kwaajili ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Katika kutekeleza jukumu hilo, Tume inatangaza nafasi za kazi ili kupata Watendaji watakaosimamia zoezi hilo. Kazi hizo ni zifuatazo:-
✅Mratibu wa Uandikishaji (Nafasi moja Unguja na Nafasi moja Pemba)
MAJUKUMU:-
- Kuratibu habari na taarifa mbalimbali za Uandikishaji.
- Kuratibu upatikanaji wa vifaa na nyenzo zinazohitajika katika kufanikisha Uandikishaji/Uboreshaji.
- Kuwa kiungo kati ya Tume, Watendaji wa shughuli za Uandikishaji katika Wilaya/Majimbo na Wadau.
- Kushirikiana na kushauriana na Maafisa Uandikishaji waliopo katika eneo lake.
SIFA ZA MRATIBU WA UANDIKISHAJI:-
- Awe raia wa Tanzania.
- Awe Mtumishi wa Umma.
- Awe na Shahada au Stashahada ya Juu au Stashahada katika fani yoyote.
- Awe muadilifu na mwaminifu.
- Awe mkazi wa eneo husika (Pemba au Unguja)
- Awe tayari kujituma na kuweza kufanya kazi bila ya kusimamiwa kwa karibu.
- Awe na uzoefu katika masuala ya Uandikishaji wa Wapigan Kura/Uchaguzi
✅Afisa Mwandikishaji (Nafasi moja kwa kila Wilaya)
MAJUKUMU
- Kuratibu na kusimamia shughuli za Uandikishaji katika Wilaya yake.
- Kusimamia na kufuatilia utendaji kazi wa Watendaji wa Uandikishaji walio chini yake.
- Kutunza vifaa vya Uboreshaji katika Wilaya husika.
- Kusimamia matumizi ya fedha za Uandikishaji.
- Kushirikiana na kushauriana na Mratibu wa Uandikishaji katika kuleta ufanisi kwenye shughuli za Uandikishaji/Uboreshaji.
- Kutoa taarifa ya mwenendo wa hatua za uandikishaji kwa kuzingatia maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
NAFASI za Kazi Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi August 14-2024
SIFA ZA AFISA MWANDIKISHAJI
- Awe raia wa Tanzania.
- Awe mtumishi wa Umma.
- Awe na Shahada au Stashahada ya juu au Stashahada katika fani
yoyote. - Awe muadilifu na mwaminifu.
- Awe tayari kujituma na kuweza kufanya kazi bila wa karibu.
ya usimamizi - Awe na uzoefu katika masuala ya Uandikishaji/Uchaguzi.
✅Afisa Mwandikishaji Msaidizi Ngazi ya Jimbo (Nafasi tatu kwa kila Jimbo)
MAJUKUMU
- Kuwa kiungo kati ya Jimbo na Wilaya.
- Kusimamia shughuli zote za Uandikishaji katika Jimbo husika.
Kumsaidia Afisa Mwandikishaji katika masuala yote ya Uandikishaji. - Awe raia wa Tanzania.
- Awe ni Mtumishi wa Umma.
- Awe na Shahada au Stashahada ya juu au Stashahada katika fani yoyote.
- Awe tayari kujituma na kuweza kufanya kazi bila ya usimamizi wa karibu.
- Awe na Uzoefu katika masuala ya Uandikishaji/Uchaguzi.
- Awe muadilifu na mwaminifu.
Kila Mwombaji katika nafasi husika aainishe nafasi anayoiomba akitaja Wilaya au Jimbo analotaka kufanyia kazi na aambatishe maelezo ya taarifa binafsi (CV).
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 27 Agosti, 2024 saa 9:30 Alasiri.
Barua zote zielekezwe kwa:
Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,
Ofisi ya Zanzibar,
Mtaa wa Maisara,
S. L. P. 4670,
ZANZIBAR.
MUHIMU: Maombi yote yatapokelewa katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo Maisara kwa upande wa Unguja na Chake Chake kwa upande wa Pemba.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF
Tags: NAFASI za Kazi Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi August 14-2024