NAFASI za Msaidizi wa Kumbukumbu kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024
NAFASI za Msaidizi wa Kumbukumbu kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024
NAFASI za Msaidizi wa Kumbukumbu kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024, Nafasi za Msaidizi wa Kumbukumbu Kutoka Halmashauri Wilaya ya Shinyanga Leo July 04-2024, Ajira za Mpya Kutoka Halmashauri Wilaya ya Shinyanga July 04-2024.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga amepokea Kibali cha Ajira Mpya kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia Barua yenye Kumb.Na.FA.97/228/01/09 ya tarehe 25.06.2024.
Hivyo, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi zifuatazo:
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (NAFASI 02)
SIFA ZA KUAJIRIWA.
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI). Awe na Stashahada (NTA level 6) katika fani ya Masjala kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.
KAZI NA MAJUKUMU YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II
- Kuorodhesha barua zinazoingia Masjala kwenye regista (incoming
correspondence register);Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (outgoing correspondence register); - Kusambaza majalada kwa Watendaji (action officers);
- Kupokea majalada kwa Watendaji ( action officers);
- Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa Watendaji;
- Kurudisha majalada kwenye shabaka/kabati la majalada(racks/filling cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa; na
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking).
MSHAHARA Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
- Waombaji wawasilishe maelezo binafsi (Curriculum Vitae) yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye Anuani na Namba za simu za kuaminika pamoja na majina
ya wadhamini watatu (Referees) wa kuaminika. - Waombaji waambatanishe nakala za vyeti vya Kidato cha Nne au Sita, Taaluma na cheti cha kuzaliwa. Waombaji watakaowasilisha” Result Slip”,” Statement of
Results”,” Provisional Results” au” Transcripts HAVITAKUBALIKA. - Kwa Waombaji waliosoma nje ya Nchi, Elimu ya Kidato cha Nne au Sita wawasilishe uthibitisho kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
- Kwa waombaji waliosoma Vyuo nje ya Nchi wawasilishe uthibitisho kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
- Waombaji watakokidhi sifa zinazotakiwa ndio watakaoitwa katika usaili.
- Barua ya maombi iliyosainiwa na Mwombaji inaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiingereza au Kiswahili.
- Waombaji wenye mahitaji maalum (special needs/disability) wanatakiwa kuainisha kwenye maombi yao.
- Waombaji watakaowasilisha Taarifa za kughushi watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria za Nchi.
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 18 Julai, 2024.Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 2 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga More Details |
2024-07-18 Login to Apply |
Tags: Ajira za Mpya Kutoka Halmashauri Wilaya ya Shinyanga July 04-2024., Nafasi za Msaidizi wa Kumbukumbu Kutoka Halmashauri Wilaya ya Shinyanga Leo July 04-2024, NAFASI za Msaidizi wa Kumbukumbu kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024