NAFASI za Mwandishi Mwendesha Ofisi Manispaa ya Tabora June 01-2024
NAFASI za Mwandishi Mwendesha Ofisi Manispaa ya Tabora June 01-2024
NAFASI za Mwandishi Mwendesha Ofisi Manispaa ya Tabora June 01-2024, NAFASI za Kazi Kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Tabora June 01-2024, Ajira Mpya kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Tabora June 01-2024.
- MAJINA ya Walioitwa Kujiunga na Mafunzo ya JKT 2024
- MAJINA 500 ya Walioitwa Kwenye Mafunzo Jeshi la Magereza Tanzania June 03-2024
Kufuatia Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kupata kibali cha Ajira Mbadala chenye Kumb.Na.FA.228/613/01/B/010 cha tarehe 22 April, 2024 kwa nafasi ya
Mwandishi Mwendesha Ofisi II kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu ajira mpya, Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Mansipaa ya Tabora anatangaza nafasi ya kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi kama zilivyoorodheshwa katika tangazo hili:-
MWANDISHI MWENDESHA OFISI II – NAFASI MOJA (1)
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye elimu ya Kidato cha Nne (Form Four) au Kidato cha Sita (Form Six) aliyehitimu mafunzo ya Stashahada/Diploma (NTA level 6) ya Uhazili na awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata
programu za kompyuta za ofisi kama vile Word, Excel, Powepoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri;
- Kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaeleza wanapoweza
kusaidiwa; - Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi;
- Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa waliokatika Idara/Kitengo/Sehemu husika;
- Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi; na
- Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali TGS C kwa Mwezi
MASHARTI YA UJUMLA
- Mwombaji awe Raia wa Tanzania ambaye ana umri si zaidi ya miaka 45 na siyo pungufu ya miaka 18.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji waambatashe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) yenye Anwani inayotumika, namba ya simu na Anuani ya barua pepe (Email address) pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika
- “Provisional/Testimonials/Statement of results” na hati za matokeo za kidato cha nne na sita (form IV na VI result slip) HAVITAKUBALIKA
- Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokua kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma, wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NACTE na NECTA)
- Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria
- Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni Jumamosi, tarehe 16 JUNI, 2024
MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa Mkurugenzi
Halmashauri ya Mansipaa yaTabora,
S.L.P 174
TABORA
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa Ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https:portal.ajira.go.tz/ (anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa
‘Recruitment Portal’)
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katka Tangazo hili HAYATAFIKIRIWA
POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 1 POST Employer: Halmashauri ya Manispaa ya Tabora More Details |
2024-06-14 Login to Apply |
Tags: Ajira Mpya kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Tabora June 01-2024., NAFASI za Kazi Kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Tabora June 01-2024, NAFASI za Mwandishi Mwendesha Ofisi Manispaa ya Tabora June 01-2024
Community development officer