NAFASI za Watendaji Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC 2024
NAFASI za Watendaji Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC 2024
NAFASI za Watendaji Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC 2024,Nafasi za kazi Tume ya Uchaguzi 2024,Nafasi za kazi tume ya uchaguzi zanzibar 2024,Nafasi za kazi uchaguzi,Ajira portal,Tume ya uchaguzi tanzania.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imetangaza nafasi za kazi za watendaji wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Kwahani utakaotanyika siku ya a Jumamosi tarehe 8 June 2024.
Kwa mujibu wa Tangazo lililosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Tume inatarajia kuendesha Uchaguzi Mdogo wa Mbunge wa Jimbo la Kwahani, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar tarehe 08 June 2024.
Katika kutekeleza jukumu hilo, Tume inatangaza nafasi za kazi ili kupata Watendaji watakaosimamia zoezi hilo. Nafasi za kazi hizo ni kama zifuatazo: –
1.Msimamizi wa Uchaguzi (Nafasi moja)
MAJUKUMU
- Kuratibu na kusimamia shughuli za Uchaguzi katika Wilaya husika.
- Kusimamia na kufuatilia utendaji kazi wa Watendaji wa Uchaguzi walio chini yake.
- Kutunza vifaa vya Uchaguzi katika Wilaya husika. 4. Kusimamia matumizi ya fedha za Uchaguzi.
- Kushirikiana na kushauriana na Mratibu wa Uchaguzi katika kuleta ufanisi kwenye shughuli za Uchaguzi.
- Kutoa taarifa ya mwenendo wa hatua za uchaguzi kwa kuzingatia maelekezo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
SIFA ZA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI
- Awe raia wa Tanzania.
- Awe mtumishi wa Umma.
- Awe na Shahada au Astashahada katika fani yoyote.
- Awe mkazi wa Wilaya husika.
- Awe muadilifu na mwaminifu.
- Awe tayari kujituma na kuweza kufanya kazi bila ya usimamizi wa karibu.
- Awe na uzoefu katika masuala ya Uchaguzi/Uandikishaji wa Wapiga Kura.
- Ndani ya miaka mitano awe hajawahi kutiwa hatiani katika shauri la nidhamu au kosa lolote la jinai na kuadhibiwa kwa kifungo kinachozidi miezi sita.
- Awe hajawahi kuwa kiongozi wa chama cha siasa kwa kipindi cha miaka mitano.
2:Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Jimbo (Nafasi mbili)
MAJUKUMU
- Kusimamia shughuli zote za Uchaguzi katika Jimbo husika.
- Kumsaidia Msimamizi wa Uchaguzi katika masuala yote ya Uchaguzi.
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe raia wa Tanzania.
- Awe ni Mtumishi wa Umma.
- Awe na Shahada au Stashahada ya juu au stashahada katika fani yoyote.
- Awe mkazi wa Wilaya husika.
- Awe tayari kujituma na kuweza kufanya kazi bila ya usimamizi wa karibu.
- Awe na Uzoefu katika masuala ya Uchaguzi/Uandikishaji wa Wapiga Kura.
- Awe muadilifu na mwaminifu.
- Awe hajawahi kutiwa hatiani katika shauri la nidhamu au kosa lolote la jinai na kuadhibiwa kwa kifungo kinachozidi miezi sita.
- Awe hajawahi kuwa kiongozi wa chama cha siasa.
Kila Mwombaji katika nafasi husika aainishe nafasi anayoiomba na aambatishe maelezo ya taarifa binafsi (CV) akiweka Jina la Taasisi anayofanyia kazi na cheo chake.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 07 Mei, 2024 saa 9:30 Alasiri.
Barua zote zielekezwe kwa:
Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,
Ofisi ya Zanzibar,
Mtaa wa Maisara
S. L. P. 4670,
Zanzibar.
MUHIMU: Maombi yote yatapokelewa katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo Maisara, Unguja.
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar iliundwa kwa mujibu wa kifungu cha 119(1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 pamoja na kifungu cha 4 cha Sheria ya Uchaguzi Nam.11 ya 1984. Tume ya uchaguzi ya Zanzibar iliundwa tarehe 26 Machi, 1993 ikiwa na mwenyekiti ambaye ameteuliwa na Rais wa Zanzibar na Makamo mwenyekiti aliyechaguliwa na Wajumbe wa Tume kutoka miongoni mwa Wajumbe sita wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar walioteuliwa na Mheshimiwa Rais.
Uteuzi wa Wajumbe wa Tume unadumu kwa kipindi cha miaka mitano tangu mjumbe alipoteuliwa ambapo Tume hii ni ya mwanzo kwa Zanzibar kuteuliwa kuendesha na kusimamia Uchaguzi kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ambayo imeteuliwa tarehe 26 Machi,1993 na kumaliza kipindi chake cha cha miaka mitano ya utumishi tarehe 25 Machi,1998.
WAJUMBE WA MWANZO WA TUME.
Wajumbe wafuatao wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar waliteuliwa na Rais wa Zanzibar DK. SALMIN AMOUR JUMA tarehe 26 Machi,1993 :-
1. | Mwinyiwesa Idarous | Mwenyekiti |
2. | Ussi Khamis Haji | Makamo Mwenyekiti |
3. | Ahmada Khamis Hilika | Mjumbe |
4. | Hassan Haji Ali | Mjumbe |
5. | Issa Omar Suleiman | Mjumbe |
6. | Hassan Said Mzee | Mjumbe |
7. | Moza Himid Mbaye | Mjumbe |
Tarehe 21 Machi, 1995 Mhe. Mwinyiwesa Idarous na Mhe.Ussi Khamis Haji walijiuzulu kutokana na tuhuma za baadhi ya vyama vya siasa kwamba Tume imeelemea kwenye Chama tawala na hasa Mwenyekiti wake. Tuhuma hizi dhidi ya Tume zilipewa uzito na nguvu na baadhi ya wafadhili kutoka nje. Mhe.Rais wa Zanzibar alimteua Mhe. Zubeir Juma Mzee kuwa Mwenyekiti na Mhe. Ahmed Mohammed AbdulRahman kuwa mjumbe wa Tume kushika nafasi zilizoachwa wazi na Wajumbe waliojiuzulu.
Nafasi ya makamo mwenyekiti ilichukuliwa na Mhe. Hassan Said Mzee baada ya aliyekuwa makamo mwenyekiti kujiuzulu na kuteuliwa mjumbe mwengine wa Tume.
Tags: Ajira portal, Nafasi za kazi tume ya uchaguzi 2024, Nafasi za kazi tume ya uchaguzi zanzibar 2024, Nafasi za kazi uchaguzi, NAFASI za Watendaji Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC 2024, Tume ya uchaguzi tanzania