RASMI Chadrack Issaka Boka ni Mwananchi
RASMI Chadrack Issaka Boka ni Mwananchi
RASMI Chadrack Issaka Boka ni Mwananchi,Klabu ya Yanga usajili wa beki wa kushoto, Chadrack Issaka Boka kutoka FC Saint Eloi Lupopo ya nchini DR Congo.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye ni mzaliwa wa Kinshasa nchini DR Congo, anakuja kuimarisha eneo la ulinzi upande wa kushoto akisaidiana na Nickson Clement Kibabage.
Ubora wa beki huyo hauna mashaka kutokana na kwamba ndani ya kikosi cha FC Saint Eloi Lupopo alikuwa panga pangua kikosi cha kwanza.
Nyota huyo pia amekuwa akiitumikia Timu ya Taifa ya DR Congo ambapo alijumuishwa kwenye kikosi kilichoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) iliyofanyika Algeria mwaka 2022.
Katika michuano hiyo ambayo DR Congo ilikuwa Kundi B, Boka alicheza mechi zote tatu hatua ya makundi dhidi ya mabingwa Senegal, Ivory Coast na Uganda.
Usajili wa Boka ni muendelezo wa kuimarisha kikosi Cha Young Man kuelekea msimu ujao wa 2024/2025 ambapo malengo yao ni kutetea mataji yao yote ya Ligi Kuu ya NBC na Kombe la Shirikisho la CRDB Bank.
Sambamba na hilo, pia Yanga Ina malengo ya kubeba Ngao ya Jamii na kufika mbali Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya msimu uliopita 2023/2024 kuishia hatua ya robo Fainali.
Usajili wa Chadrack Boka unaifanya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji wapya watatu Kuelekea Msimu Mpya wa 2024/2025 ambapo awali alisajiliwa Kiungo, Clatous Chama na Mshambuliaji Prince Dube.
Pia Klabu hiyo imewaongezea mikataba Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery, Nickson Kibabage na Bakari Nondo
Mwamnyeto pamoja na Farid Mussa.