SABABU za Kukataliwa Kuandikishwa
SABABU za Kukataliwa Kuandikishwa
SABABU za Kukataliwa Kuandikishwa
- Mwandishi msaidizi anaweza kukataa kumwandikisha mwombaji iwapo ataridhika kuwa mwombaji hana sifa za kuandikishwa kuwa mpiga kura.
- Endapo mwandishi msaidizi atakataa kumwandikisha mwombaji chini ya kanuni ndogo ya (1) na ikiwa mwombaji atahitaji, mapema inavyowezekana, atapaswa kumueleza sababu za kukataa kumwandikisha kwa kujaza Fomu Na. 3A iliyoainishwa katika Jedwali la Kwanza.
- Ndani ya siku saba baada ya kupokea sababu ya kukataliwa, mwombaji ambaye hataridhika na uamuzi wa mwandishi msaidizi anaweza kuwasilisha kwa afisa mwandikishaji Fomu Na. 3A iliyojazwa kwaajili ya mapitio ya uamuzi wa mwandishi msaidizi.
- Afisa mwandikishaji atatoa uamuzi wa maombi ya mapitio ndani ya siku kumi na nne baada ya kupokea maombi hayo.
- Baada ya kupokea Fomu Na. 3A iliyojazwa ipasavyo, afisa mwandikishaji ataamua iwapo mwombaji ana sifa au hana sifa za kuandikishwa kama mpiga kura na kumfahamisha mwombaji ipasavyo.
- Mwombaji ambaye hataridhika na uamuzi wa afisa mwandikishaji anaweza kukata rufaa Mahakama ya Mwanzo ndani ya siku kumi na nne baada ya uamuzi kutolewa.
- Mahakama ya Mwanzo itatoa uamuzi wa rufaa ndani ya siku kumi na nne tangu siku rufaa ilipowasilishwa.
- Uamuzi wa Mahakama ya Mwanzo utakuwa ni wa mwisho.