SIFA za Mwandishi Msaidizi wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
SIFA za Mwandishi Msaidizi wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
SIFA za Mwandishi Msaidizi wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, Kwa Madhumuni ya Kanuni ndogo ya (1)
Mtu anaweza kuteuliwa kuwa Mwandishi Msaidizi au Mwendeshaji wa Kifaa cha bayometriki ikiwa atakuwa na sifa zifuatazo:
- Awe ni raia wa Tanzania;
- Awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane;
- Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha nne au zaidi na
- Awe anajua kusoma na kuandika katika lugha ya Kiswahili au Kiingereza;
Awe ni mkazi wa kata anayoomba kuwa mwandishi msaidizi au mwendeshaji wa kifaa cha bayometriki; - Awe si kiongozi au kada wa chama cha siasa; na
- Awe ni mwadilifu na mtiifu.
Kabla ya kuanza Utekelezaji wa majukumu, Mwandishi Msaidizi au Mwendeshaji wa kifaa cha bayometriki-
- Atatoa tamko la kujitoa uanachama au kutokuwa mwanachama wa chama cha siasa mbele ya afisa mwandikishaji au afisa mwandikishaji msaidizi kwa kutumia Fomu Na. 6 iliyoainishwa katika Jedwali la Kwanza; na
- Ataapa kiapo cha kutunza siri mbele ya afisa mwandikishaji au afisa mwandikishaji msaidizi kwa kutumia Fomu Na. 7 iliyoainishwa katika Jedwali la Kwanza.
Bila kujali masharti ya kanuni ndogo ya (2) (d), Tume inaweza kutoa maelekezo kwa afisa mwandikishaji kuteua mtu mwingine yeyote kuwa mwandishi msaidizi au mwendeshaji wa kifaa cha bayometrikik adri itakavyoonekana ni muhimu
Tags: SIFA za Mwandishi Msaidizi wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura