SIMBA na Yanga Kutoshiriki CECAFA Kagame Cup 2024
SIMBA na Yanga Kutoshiriki CECAFA Kagame Cup 2024
SIMBA na Yanga Kutoshiriki CECAFA Kagame Cup 2024, Rasmi Klabu za Simba na Yanga hazitashiriki Michuano ya CECAFA Kagame Cup inayotarajiwa kuanza Julai 06 jijini Dar es salaam.
Sababu za Vilabu hivyo Kutoshiriki Michuano hiyo ni kuwa katika maandalizi ya pre-season ambapo mwishoni mwa wiki hii huenda vikosi hivo vikaondoka Jijini Dar es salaam Simba ikielekea Misri na Yanga Kuelekea ambako itaweka Kambi.
Kulingana na orodha mpya ya timu zitakazoshiriki michuano hiyo iliyotolewa ikishirikisha timu za Afrika Mashariki na Kati, Simba na Yanga ni miongoni mwa timu ambazo hazipo kwenye orodha hiyo.
Aidha timu nyingine ya Tanzania, Azam FC tayari walishajiondoa Kushiriki Michuano hiyo.
Kwa jinsi hiyo timu za Coastal Union na Singida Big Stars ndizo timu pekee zitakazoshiriki kwa upande wa Tanzania Bara hyku JKU ikiiwakilisha Zanzibar.
Hii hapa ni Orodha Mpya ya timu zitakazoshiriki Michuano hiyo ambayo droo yake inatarajiwa Kufanyika Leo Jumatano Julai 3, 2024 Kuanzia Saa 6:00 Mchana Jijini Dar Es Salaam.
1:Coastal Union – Tanzania.
2:Singida Black Stars – Tanzania.
3:Gor Mahia FC – Kenya.
4: Express FC – Uganda.
5:SC Villa – Uganda.
6: Djibouti Telkom – Djibouti.
7:Dekadaha FC – Somalia.
8:El Mereikh Bantiu – Sudan Kusini.
9:Al Hilal FC – Sudan Kusini.
10:Ali Wadi FC – Sudan Kusini.
11:JKU FC – Zanzibar.
12: APR FC – Rwanda.