TAARIFA Muhimu Kwa Walioitwa kwenye Usaili Kada za Afya
Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma inawataarifu wale wote walioitwa kwenye usaili wa Kada za Afya kuwa USAILI WA KUANDIKA/ MCHUJO utafanyika Katika Mkoa ambao msailiwa anaishi kwa sasa (Current address) na USAILI WA MAHOJIANO YA ANA KWA ANA utafanyika Katika Mkoa uliochagua wakati
unaomba kazi.
Mfano kama uliomba nafasi ya Tabibu Mkoa wa Mara, utafanyia usaili wa mahojiano Katika mkoa wa Mara.
Aidha Wasailiwa wote wanatakiwa kufika wakiwa wamevaa Barakoa (MASK) Wasailiwa wote wanakumbushwa kufika na vyeti vyao halisi (Original Certificates) Wasailiwa wote wanatakiwa kufika na vitambulisho vyao.
Tags: TAARIFA Muhimu Kwa Walioitwa kwenye Usaili Kada za Afya