RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


USAJILI Karaboue Chamou ni Mnyama

Filed in Michezo, Usajili by on 07/07/2024

USAJILI Karaboue Chamou ni Mnyama

USAJILI Karaboue Chamou ni Mnyama

USAJILI Karaboue Chamou ni Mnyama

USAJILI Karaboue Chamou ni Mnyama, Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa mlinzi wa kati Karaboue Chamou raia wa Ivory Coast kutoka klabu ya Racing Club d Abidjan kwa mkataba wa miaka miwili.

Karaboue mwenye urefu wa futi 6.2 akiwa na Umri wa miaka 24 yuko vizuri kwenye kucheza mipira ya juu kuzuia na kushambulia.

Moja ya eneo ambalo lilikuwa changamoto kubwa msimu uliopita ilikuwa ulinzi na ujio wa Karaboue ni moja ya tiba hiyo.

Karaboue anakuja kuongeza nguvu katika idara ya ulinzi wa kati ambapo atashirikiana na Che Fondoh Malone na Abdulrazack Mohamed Hamza.

Karaboue Chamou anakuwa Mchezaji wa 11 kusajiliwa na Simba kuelekea msimu ujao wa Ligi wa 2024/2025 baada ya kukamilisha usajili wa Wachezaji wengine ambao ni;

Valentin Nouma kutoka St. Eloi Lupopo ya DR Congo,Omary Omary Kutoka Mashujaa FC, Debora Fernandes Mavambo Kutoka Mutondo Stars ya Zambia, Augustine Okejepha Kutoka Rivers United ya Nigeria, Valentino Mashaka Kutoka Geita Gold FC na Abdulrazack Mohamed Hamza kutoka Super Sport ya Afrika Kusini.

Wengine ni Lameck Lawi kutoka Coastal Union, Joshua Mutale kutoka Power Dynamos, Steven Mukwala kutoka Asante Kotoko na Jean Charles Ahoua kutoka Stella Club d’Adjamé.

Tags:

Comments are closed.