WACHEZAJI Simba Wafanyiwa Vipimo
WACHEZAJI Simba Wafanyiwa Vipimo
WACHEZAJI Simba Wafanyiwa Vipimo, Kikosi Cha Simba kimefanyiwa vipimo vya afya katika Hospitali ya Saifee jijini Dar es Salaam ili kujua utimamu wa mwili kabla ya kuanza maandalizi ya msimu wa 2024/2025.
Vipimo hivyo vimegawanyika katika sehemu kuu tatu ambayo ni damu, mapafu na moyo pamoja na kupima utimamu wa misuli na mishipa.
Daktari wa timu, Edwin Kagabo amesema kuwa vipimo hivyo vitalisaidia benchi la ufundi kujua wanatakiwa kupanga vipi programu za
mazoezi kwa wachezaji kulingana na utimamu wa miili yao.
Dkt. Kagabo ameongeza kuwa huu ni utaratibu wa Klabu hiyo kufanya vipimo kwa wachezaji wote kabla ya kuanza maandalizi ya msimu ili kujua hali ya utimamu wao.
“Tumewafanyia vipimo wachezaji wetu wote ili kujua utimamu wa miili yao kabla ya kuanza maandalizi ya msimu na hili ni jambo ambalo tunalifanya kila msimu unavyokaribia kuanza.”
“Wachezaji wamepimwa kila kitu kuanzia damu, moyo, mapafu na utimamu wa misuli na hii italisaidia benchi la ufundi kupanga programu za mazoezi,” amesema Dkt. Kagabo.