YANGA Yazindua Mfumo Mwingine wa Kupata Habari
YANGA Yazindua Mfumo Mwingine wa Kupata Habari
YANGA Yazindua Mfumo Mwingine wa Kupata Habari, Klabu ya Young Africans SC imezindua mfumo mwingine mpya wa kupata habari ujulikanao kwa jina la Yanga Habari.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Young Africans SC, Ally Kamwe wakati akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo.
“Leo tumezindua mfumo mpya wa kupata habari ujulikano kama Yanga habari. Haijalishi una simu ya namna gani lakini unaweza kupewa taarifa na Klabu ya Yanga. Ukijiunga na mfumo huu utapata ujumbe kutoka Klabu ya Yanga ikikuoa taarifa mbalimbali.
“Gharama za kupata Yanga Habari kwa wiki ni Tsh 500 na kwa mwezi Tsh 2000. Hii ndio njia sahihi kwa
mwanachama na shabiki wa kupata habari za uhakika na haraka. Kwanza hakikisha una salio la Tsh 100 kwenye simu yako. Piga *149*40# kwa
mitandao yote. Kisha chagua Yanga Habari, chagua vifurushi, weka namba ya siri,” alisema Kamwe.
Kabla ya kuzinduliwa kwa mfumo huo mpya, mashabiki na wanachama wa Young Africans walikuwa wakipata
habari kuhusu klabu yao kupitia mitandao ya kijamii na application ambapo sasa imeongezwa njia nyingine lengo likiwa ni kutanua wigo wa kusambaza habari za Klabu hiyo.