RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


YANGA Yatangaza Bajeti yake 2024/2025

Filed in Michezo by on 09/06/2024

YANGA Yatangaza Bajeti yake 2024/2025

YANGA Yatangaza Bajeti yake 2024/2025, Bajeti ya Yanga Msimu wa 2024/2025, hii hapa bajeti ya Yanga 2024/2025, Bajeti ya Yanga 2024/25 ni Bilioni 24.5.

YANGA Yatangaza Bajeti yake 2024/2025

YANGA Yatangaza Bajeti yake 2024/2025, Bajeti ya Yanga Msimu wa 2024/2025, hii hapa bajeti ya Yanga 2024/2025, Bajeti ya Yanga 2024/25 ni Bilioni 24.5.

Klabu ya Yanga imetenga bajeti ya Tsh Bilioni 24.5 kwa msimu mpya wa 2024/2025 ambapo imeongezeka asilimia kumi tofauti na Matumizi ya Msimu uliopita ambayo ilikuwa Bilioni 22.

Hayo yamewekwa wazi katika Mkutano Mkuu wa Wanachama uliofanyika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Julius Nyerere Leo Jumapili tarehe 9 Juni 2024.

Bajeti ya msimu uliopita ilikuwa Tsh Bilioni 21.19 na Matumizi yalikuwa Tsh Bilioni 22.109 na hivyo kuwa hasara ya Tsh Bilioni 1.09

Aidha Wanachama wa Yanga wamepitisha Bajeti ya mwaka ujao wa fedha Tsh Bilioni 24.5.

Klabu hiyo imetaja Mapato ya Yanga Msimu 2023/2024 kuwa ni;

  • Udhamini na haki za Matangazao bilioni 10.19
  • Mapato mlangoni bilioni 1
  • Ada za Wanachama milioni 613
  • Zawadi za ushindi bilioni 3.9
  • Mapato mengine bilioni 5

Jumla ya mapato Kwa Msimu 2023/2024 ni Bilioni 21.

Kupitia Mkutano huo Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amewaahidi Mashabiki na Wanachama wa Yanga kuwa watafanya usajili mkubwa sana msimu ujao.

“Msimu ujao tutafanya mambo makubwa kuanzia ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Tutafanya Pre season nzuri, tumeshapata mialiko maeneo mbalimbali ikiwemo AFRIKA KUSINI, Kaizer Chiefs wametoa mwaliko na Mh.Raila Odinga ametuomba tuungane nao kwenye uzinduzi wa Uwanja wao huko Kisumu pamoja na nchi moja ya ulaya” Injinia Hersi Said

“Klabu yetu inahitajika kujengeka kiuchumi. Kazi yetu kama viongozi ni kuhakikisha tunapata wadhamini ambaye atasaidia na mfadhili wetu GSM. Lakini mashabiki wetu pia wanao mchango mkubwa kwa kuhakikisha kuwa kupitia ada za Wanachama tunapata mapato ya kuendesha klabu yetu” Injinia Hersi Said

“Tulifanikiwa kurejea hatua ya makundi ligi ya Mabingwa AFRIKA baada ya miaka 25. Watu wengi walidhani kuwa hatutaweza kufika hatua ya robo fainali kwa sababu tulikuwa kwenye kundi gumu sana. Lakini tukawashangaza wale waliotukatia tamaa.

Tulifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali na kutolewa kwa matuta na Bingwa wa AFL na kigogo wa soka AFRIKA KUSINI, Mamelodi Sundowns. Hata hivyo katika mchezo tulifunga bao halali ambalo Rais wa Soka AFRIKA, Dr.Patrice Motsepe amenukuliwa akisema kuwa lilikuwa goli halali” Rais wa Young Africans SC Injinia Hersi Said

“Leo tupo na Mheshimiwa Mchengerwa, na tayari amepokea maombi yetu kuhusu mchakato wetu wa ujenzi wa Uwanja wetu hapa Jangwani. Jambo la kheri ni kuwa amejumuika nasi moja kwa moja akitokea Tabora. Mradi wetu huu wa ujenzi wa Uwanja tayari upo ofisini kwake na analifanyia kazi.

Mdhamini na mfadhili wetu GSM yupo tayari kutekeleza mradi wa ujenzi wa uwanja. Kwa bahati mbaya, GSM hajawahi kutoa ahadi hewa. Hivyo niwaahidi wanachama na mashabiki wetu kuwa mchakato wetu upo tayari kuanza kwa kuzingatia mradi wa mto Msimbazi” Injinia Hersi Said

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Mohamed Mchengerwa amewashukuru Viongozi wa Young Africans Kwa kumualika kwenye Mkutano huo na kusema!

“Nawashukuru sana Young Africans SC kwa kunialika kwenye mkutano wenu huu mkuu. Ni heshima kujumuika nanyi ikiwa nyie ni Klabu yenye mafanikio makubwa sana. Nafikisha salamu za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa chachu kwenye maendeleo ya soka nchi hii” Mgeni Maalum Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa

“Mafanikio ya leo ya Yanga, kuna watu walifanya kazi kubwa kuhakikisha klabu hii inatulia. Utulivu wa Yanga ndio maendeleo ya soka letu. Mafanikio ya Yanga leo ni kwa sababu ya Injinia Hersi na wenzake walifanya kazi kwa utulivu na weledi mkubwa. Hongera sana Injinia Hersi kwa kufanya Klabu ya kisasa zaidi. Uwekezaji uliofanywa kwenye klabu hii imekuwa chachu ya maendeleo ya soka Tanzania. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa

“Rais Samia ameagiza zaidi bilion 400 zielekezwe kwenye mradi wa bonde la msimbazi. Mradi huo utaisaida sana kwenye malengo ya ujenzi wa Uwanja wa Yanga. Katika eneo hilo litajengwa daraja bora na la kisasa. Mchakato wa mradi huo utaanza mara moja na mradi wa Yanga utakuwa sehemu ya mradi huo.

Nimemwagiza mtendaji mkuu anayehusika na kuendeleza mradi wa mto msimbazi aonane mara moja na maofisa wa Yanga kukamilisha mchakato. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa

Kwa Upande wa Waziri wa Sanaa tamaduni na michezo Mhe. Dkt. Damasi Ndumbaro amewapongeza Yanga Kwa kupiga hatua kubwa sana kwenye maendeleo ya Soka.

“Tukiondoa ushabiki wetu, Yanga wamepiga hatua kubwa sana kwenye maendeleo ya soka. Nasema hivi ili vilabu vingine vipate wivu. Jambo hili halijatokea kama uyoga, tuwape heshima zao, Injinia Hersi na GSM. Nawasihi wanayanga wawalinde hawa watu kwa wivu mkubwa sana. Asije mtu akatokea na njaa zake akawarudisha mlikotoka. Ile klabu yangu mimi, bundi amehamia sasa hivi” Waziri wa Sanaa tamaduni na michezo Mhe. Dkt. Damasi Ndumbaro

Gerson Msigwa ambaye ni Katibu Wizara ya Utamaduni sanaa na Michezo yeye aliwapongeza Yanga Kwa Mafanikio waliyoyapata

“Kwa dhati ya moyo wangu naipongeza Yanga SC kwa mafanikio makubwa ndani na nje ya mipaka ya nchi. Yanga SC mmetengeneza weledi katika namna ya uendeshaji wa timu. Sisi kama Serikali tunatamani vilabu vijiendeshe kwa utulivu ili soka la Tanzania likue” Gerson Msigwa – Katibu Wizara ya Utamaduni sanaa na Michezo

 

“Michezo kwa sasa ni sayansi tu hakuna tena makando kando yasiyo na tija. Kwa sasa ukiitazama Yanga unaona “Pure Science” Natamani kuona vilabu vingine vikiiga namna ya kuendesha soka”

“Ninachowasisitiza Yanga ni kukwepa migogoro. Najua Yanga haina migogoro ila nasisitiza kwa vilabu vingine kuachana na migogoro. Kinachofanya Yanga isiwe na migogoro kwa sasa wanaendesha klabu kwa weledi. Viongozi makini hawagombani bali wanatafuta suluhu” Gerson Msigwa

Katika hali nyingine ile Surprise ilikuwa ya Kocha Miguel Gamondi ambaye ameongeza miaka miwili ya kuendelea kuwa kocha mkuu wa Yanga SC hadi mwaka 2026.

Haya ni Mafanikio ya Miguel Gamondi Msimu mmoja akiwa Yanga SC

🏆 Ligi Kuu ya NBC 1x (30th Club record)
🏆 CRDB FA Cup 1x
🏆 Robo Fainali #CAFCL
⚽️ Magoli 115 mashindano yote (Record)
2️⃣ Top Scorers (Ki Azizi PL & Mzize FA Cup)
🛑 Unbeaten – CRDB FA Cup

Tags: , , ,

Comments are closed.