MAJUKUMU ya Afisa Tarafa
MAJUKUMU ya Afisa Tarafa
MAJUKUMU ya Afisa Tarafa, Majukumu ya Afisa Tarafa Tanzania.
- NAFASI za Kazi Hospitali ya Saifee Zanzibar July 2024
- Majukumu ya Afisa Tarafa Kwenye Mamlaka ya Serikali Kuu.
- Kumwakilisha na kumsaidia Mkuu wa Wilaya katika utekelezaji wa shughuli za Serikali Kuu katika Tarafa.
- Kuandaa na kuratibu taarifa na ripoti zinazohusu masuala ya ulinzi na usalama ya kata kwenye tarafa yake na kuiwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
- Kuhamasisha na kuhimiza wananchi iliwashiriki kwenye shughuli za maendeleo kwenye Tarafa.
- Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Wananchi Katika Tarafa.
- Kuwa mlinzi wa amani katika eneo lake.
- Kufuatilia na kuhimiza utekelezaji wa sera za Serikali katika eneo lake na kuhakikisha kuwa zinatekelezwa ipasavyo.
- Kuratibu shughuli zote za maafa na dharura mbalimbali katika eneo lake.
- Kuandaa taarifa zote zinazohusu masuala ya Serikali Kuu kuhusu utendaji wa kazi za maafisa Watendaji wa kata wa eneo lake na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
- Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Serikali za Mitaa. katika eneo lake.
- Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Katibu Tawala wa Wilaya.
- Majukumu ya Afisa Tarafa Kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa;
- Kuwasaidia Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa katika shughuli za Maendeleo katika eneo lake.
- Kusimamia utendaji wa shughuli za Maafisa Watendaji wa Vijiji, Kata na Mitaa.
- Kushiriki na kutoa ushauri katika upangaji wa mipango ya Maendeleo katika eneo lake.
- Kuhudhuria vikao vya kamati za Halmashauri na Baraza la madiwani na kutoa ushauri.
- Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake kama zitakavyopokelewa kutoka kwa Watendaji wa Kata.
- Kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa au Jiji.
Tags: MAJUKUMU ya Afisa Tarafa