MAJINA ya Waajiliwa wapya wa Mkataba kada za Afya January 2024
MAJINA ya Waajiliwa wapya wa Mkataba kada za Afya January 2024
MAJINA ya Waajiliwa wapya wa Mkataba kada za Afya January 2024, Tangazo la kuitwa kazini waajiliwa wapya wa mkataba kada za Afya kupitia Mradi wa TMCHIP,ajira za afya 2023/2024, Majina Ya walioajiriwa kada ya Afya 2024, Ajira Wizara ya Afya 2024 PDF,Majina ya walioitwa kazini 2024.
Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali za kada za afya waliowasilisha maombi katika kipindi cha mwezi wa April, 2023 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi
umekamilika kwa awamu ya tatu.
Awamu hii ni kwaajili ya kujaza nafasi wazi za Watumishi waliokosa ajira awamu zote 2 za awali, Ikumbukwe kuwa Ajira hizi ni za Mkataba ya miaka miwili (2).
Hivyo wataalamu wote watakaojiriwa katika awamu hii wataingia mikataba na Wakurugenzi wa Halmashauri husika.
Mwezi Aprili, 2023 Ofisi ya Rais – TAMISEMI ilipata kibali cha ajira ya watumishi 8,070 wa kada mbalimbali za Afya. Nafasi ambazo zilipata waombaji wa kutosha na kupelekea kubaki kwa baadhi ya waombaji wenye sifa katika kanzi data ya OR TAMISEMI, kutokana na maombi kuzidi idadi ya kibali.
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya imefanikiwa kutumia kanzi data ya waombaji wenye sifa waliokuwa
wamebaki katika mfumo na kuwapangia vituo vya kazi watumishi 275 katika
Halmashauri mbalimbali.
Ieleweke kwamba ajira hizi ni za Mkataba kati ya Halmashauri
husika na mtaalamu husika.
Mkataba huu utasimamiwa na OR TAMISEMI wakati wa utekelezaji wa Mpango wa Uwekezaji katika Afya ya Mama na Mtoto yaani Tanzania
Martenity and Child Health Investment program (TMCHIP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.
Gharama za malipo ya mishahara zitazingatia taratibu za ajira Serikalini.
Waombaji wote waliopata nafasi wanatakiwa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
- Kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa katika muda wa siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili.
- Aidha, waombaji watakaoshindwa kuripoti kwenye vituo vya kazi ndani ya siku kumi na nne (14) nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine haraka iwezekanavyo.
- Kuwasilisha Vyeti Halisi (Original Certificates) vya Kidato cha Nne, Sita, Chuo Kikuu, NACTE na vyeti halisi vya usajili wa mabaraza ya kitaaluma kwaajili ya kuhakikiwa na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.
- Waombaji waliopata nafasi za ajira watakaoripoti bila ya kuwa na Vyeti Halisi (Original Certificates) vya Kidato cha Nne, Kidato Sita, Chuo Kikuu, NACTE na vyeti halisi vya usajili wa mabaraza ya kitaaluma hawatapokelewa.
- Waombaji waliopata nafasi za ajira wanajulishwa kuwa hakutakuwa na nafasi ya kubadilisha vituo vya kazi walivyopangiwa.
- Waombaji wote ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili, watambue kuwa hawakupata nafasi hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi
zitakapotangazwa. - Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wanaelekezwa kuwapokea, kuhakiki vyeti, Kuandaa na kuingia Mikataba ya ajira na wataalamu waliopangwa na kuwafanyia mafunzo elekezi (Induction Course) kabla ya kuwapangia vituo vya kazi.
Orodha ya majina ya waombaji waliopangiwa vituo vya kazi inapatikana kupitia tovuti ya OR-TAMISEMI www.tamisemi.go.tz au Kwa kudownload PDF HAPA.
Tangazo la Ajira kada za Afya (Replacement) Januari 2024
Kuona orodha bofya hapa
Tangazo la kuitwa kazini waajiliwa wapya wa mkataba kada za Afya kupitia Mradi wa TMCHIP
Kuona orodha bofya hapa
Limetolewa na:
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais – TAMISEMI,
Mji wa Serikali – Mtumba,
S.L.P. 1923,
DODOMA.
26 Januari, 2024
Majina ya walioitwa kazini TAMISEMI 2024 TAMISEMI Ajira za Afya 2024, Tangazo la Ajira TAMISEMI 2024 PDF, TAMISEMI news today ajira, www.ajira.tamisemi.go.tz2024 Wizara ya Afya Ajira, Tangazo la Ajira TAMISEMI september 2024, Ajira kada ya afya.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- MATOKEO Ya Darasa la Nne 2023/2024
- MATOKEO ya Kidato Cha Pili 2023/2024
- JINSI ya Kuangalia Matokeo Kidato Cha Nne 2023/2024
- ADA za Lipa kwa Airtel Mitandao Yote
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024
- TETESI Za Usajili Yanga SC Dirisha Dogo 2023/2024
- Ada/makato ya Lipa kwa M-pesa, Lipa kwa Simu
- TETESI Za Usajili Simba SC Dirisha Dogo 2023/2024
- ORODHA ya Vilabu Bora Afrika November 2023 (IFFHS Club Ranking)
- MSIMAMO Kundi D CAF Champions League 2023/2024
- MSIMAMO Wa Kundi B CAF Champions League Standings 2023/2024
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- MSIMAMO NBC Premier League 2023/2024
- WAFUNGAJI Wanaoongoza Magoli NBC Premier League 2023/2024
- KIKOSI cha Yanga SC msimu wa 2023/2024
- RATIBA Kamili Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Simba SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Yanga SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya England (EPL 2023/2024)
- KIKOSI cha Simba SC msimu wa 2023/2024
Tags: Ajira Wizara ya Afya 2024 PDF, ajira za afya 2023/2024, MAJINA ya Waajiliwa wapya wa Mkataba kada za Afya January 2024, Majina Ya walioajiriwa kada ya Afya 2024, Majina ya walioitwa kazini 2024, Tangazo la kuitwa kazini waajiliwa wapya wa mkataba kada za Afya kupitia Mradi wa TMCHIP