RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


JINSI ya Kujaza Fomu ya Maombi ya Pasipoti

Filed in Ajira, Makala, Michezo by on 14/07/2024

JINSI ya Kujaza Fomu ya Maombi ya Pasipoti

JINSI ya Kujaza Fomu ya Maombi ya Pasipoti,Fomu ya maombi ya passport tanzania, Maombi ya passport online, Maombi ya passport mpya Tanzania,Tanzania passport application form PDF,
Jinsi ya kuangalia Passport Online, passport application form Tanzania.

JINSI ya Kujaza Fomu ya Maombi ya Pasipoti

JINSI ya Kujaza Fomu ya Maombi ya Pasipoti,Fomu ya maombi ya passport tanzania, Maombi ya passport online, Maombi ya passport mpya Tanzania,
Tanzania passport application form PDF,
Jinsi ya kuangalia Passport Online, passport application form Tanzania.

Mfumo wa Passport

Hii ni huduma mpya inayomuwezesha muombaji kujaza Fomu ya Maombi ya Pasipoti kwa njia ya Kielektroniki akiwa mahali popote.

Baada ya kujaza fomu hiyo, atatakiwa kuichapisha (Print) na kuiwasilisha pamoja na vielelezo vingine katika Ofisi ya Uhamiaji iliyo karibu naye kwaajili ya kushughulikiwa maombi yake ya Pasipoti.

  1. Cheti cha Kuzaliwa Mwombaji
  2. Cheti/Kiapo cha Kuzaliwa Mzazi wa Mwombaji
  3. Kitambulisho cha Taifa
  4. Picha ya Mwombaji ya hivi karibuni yenye kivuli cha rangi ya buluu isiyokoza (Light blue Background)
  5. Ada ya Fomu Tsh 20,000
  6. Ushahidi wa Safari au Ushahidi wa Shughuli anayofanya Mwombaji.
  1. Bofya Anza kujaza fomu, kwa Ombi Jipya
  2. Bofya ENDELEA ili kuendelea na Ombi ambalo halikufikia mwisho
    Utahitajika Kujaza Namba ya Utambulisho (Rfeference ID) wa Ombi lako na Namba ya Ombi (Application Number) husika
  3. Jaza Taarifa zako sahihi kwa ukamilifu
  4. Hifadhi Namba yako ya Utambulisho (Application ID) kwa matumizi ya baadaye.
  5. Jaza Taarifa za Pasipoti ya zamani (ikiwa uliwahi kuwa na pasipoti)
  6. Jaza Taarifa za Wadhamini na Watu ambao ungependa wapewe taarifa endapo utatakewa na tatizo lolote
  7. Ambatanisha Vielelezo vyote vinavyohitajika (kwa kuzingatia maelekezo)
  8. Hakiki Taarifa zako zote na kisha bofya kukubaliana nazo ikiwa ziko sahihi
  9. Lipia fomu yako baada ya kupatiwa Namba ya Kumbukumbu ya Malipo (Control Number)

Kitufe cha Kufuatilia Hali (Status) ya Ombi kinakuwezesha kufuatilia Ombi lako limefikia hatua gani.

Kwa Mwombaji anayeanza kujaza fomu ya maombi ya Pasipoti kwa njia ya kielektroniki kwa mara ya kwanza (hata kama alishawahi kuwa na pasipoti).

Ombi Jipya

Kwa Mwombaji ambaye alishajaza fomu ya maombi ya pasipoti kwa njia ya kielktroniki na kufikia hatua ya kupatiwa Namba ya Ombi. Hatua hii itampa fursa ya kurekebisha taarifa zake au Kupakua na kuichapisha fomu yake. Ni hatua muhimu katika kuendeleza ombi la Mteja ambalo halikufikia hatua ya mwisho.

Endeleza Ombi

Kwa Mwombaji ambaye alishajaza fomu ya maombi ya pasipoti kwa njia ya kielktroniki na kufikia hatua ya kupatiwa Namba ya Ombi. Hatua hii itampa fursa ya kurekebisha taarifa zake au Kupakua na kuichapisha fomu yake. Ni hatua muhimu katika kuendeleza ombi la Mteja ambalo halikufikia hatua ya mwisho.

Angalia Ombi

HATUA ZA UJAZAJI FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI (MTANDAO).

  1. INGIA KATIKA TOVUTI YA IDARA: www.immigration.go.tz KISHA NENDA KATIKA KITUFE CHA e-SERVICES
  2. CHAGUA PASSPORT APPLICATION FORM;
  3. CHAGUA OMBI JIPYA;
  4. TIKI KIBOKSI KUKUBALIANA NA MAELEKEZO;
  5. JAZA TAARIFA ZAKO KWA UKAMILIFU UKIFUATA MAELEKEZO NA MPANGILIO (FORMAT) KATIKA KILA KIPENGELE;

NB:

BAADA YA MWOMBAJI KUKAMILISHA KUJAZA TAARIFA ZAKE, ATAFAHAMISHWA YA KWAMBA USAJILI UMEKAMILIKA NA KUPATIWA NAMBA YA OMBI, AMBAYO NI MUHIMU AIANDIKE PEMBENI NA KUIHIFADHI KWA KUMBUKUMBU ZA BAADAE. KISHA ATAPEWA NAMBA YA KUMBUKUMBU YA MALIPO (CONTROL NUMBER) NA KUTAKIWA KWENDA KULIPIA MALIPO YA AWALI (ADVANCE FEE) YA TSH 20,000.

BAADA YA KUKAMILISHA USAJILI, NA KUPATIWA NAMBA YA OMBI NA NAMBA YA KUMBUKUMBU (CONTROL NUMBER), UKURASA UTAONEKANA KAMA IFUATAVYO:

INGIA KWENYE MENU YA M-PESA/TIGOPESA (*150*00#/*150*01#)

  1. Bonyeza Namba 4 (Lipa kwa M-Pesa) – VODA
  2. Bonyeza Namba 4 (Kulipia Bili) – TIGO

Kisha Weka/Ingiza Namba ya Kampuni

  1. Ingiza Namba (888999)
  2. Ingiza kumbukumbu Namba(Ingiza Control Number inayoanzia na 99109…….)
  3. Ingiza kiasi (kama ulivyo elekezwa Mfano: 20,000 nk.)
  4. Utapata Maelezo kuwa unalipa pesa NMB
  5. Ingiza Namba ya Siri
  6. Hakiki
  7. Utapata Meseji toka M-Pesa/Tigopesa kama muamala umekubalika;

Utapata meseji kutoka kwenye mfumo Namba 15200
kama muamala umekubalika;

  1. Mteja atatakiwa kurudi katika OMBI LINALOENDELEA:
  2. Kisha ataingiza NAMBA YA OMBI/SIMU na NAMBA YA RISITI

Na hapo ataweza kupakua Fomu yake ya Maombi

Ataiwasilisha Fomu hiyo katika Ofisi ya Uhamiaji Makao makuu au Afisi Kuu Zanzibar

  1. Jaza fomu ya malipo ya kielectroniki;
  2. Fuata maelekezo kama yanavyojieleza kwenye fomu;
  3. Utapata meseji toka benki;

Utapata meseji toka kwenye mfumo Namba 15200 kama muamala umekubalika.

Maombi ya passport ya dharura,
Bei ya passport Tanzania Inachukua muda gani, kupata passport mpya,
www.immigration.go.tz application form, Jinsi ya kuandika barua ya kuomba passport ya kusafiria, Viambatanisho vya maombi ya passport.

Tags: , , , , , ,

Comments are closed.