JOHN Bocco arudishwa Uwanjani
JOHN Bocco arudishwa Uwanjani
JOHN Bocco arudishwa Uwanjani, Klabu ya JKT Tanzania FC imetajwa kukamilisha usajili wa Mshambuliaji, John Bocco ambaye ndiye atakayekuwa nahodha mpya wa kikosi hicho.
Bocco anatua JKT Tanzania kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kupewa Thank You na Simba, licha ya kwamba alipewa majukumu ya kukinoa kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 17 pale Msimbazi.
Aidha Wachezaji Said Ndemla na David Bryson wamesaini mikataba mipya baada ya kumaliza mikataba ya mkopo kutoka Singida Fountain Gate hivyo wataendelea kuwa sehemu ya kikosi hicho msimu ujao wa 2024/2025.
Pia mshambuliaji Charles Ilanfya kutoka Mtibwa Sugar iliyoshuka Daraja amejiunga na JKT Tanzania kwaajili ya msimu ujao wa 2024/2025.