RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


MAJINA 194 ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Mwanga 18-05-2024

Filed in Ajira, Michezo by on 18/05/2024

MAJINA 194 ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Mwanga 18-05-2024

MAJINA 194 ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Mwanga 18-05-2024, Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Leo tarehe 18-2024, Orodha ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga May 18-2024,TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA MWANGA 18-05-2024.

MAJINA 194 ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Mwanga 18-05-2024

MAJINA 194 ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Mwanga 18-05-2024, Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Leo tarehe 18-2024, Orodha ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga May 18-2024,TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA MWANGA 18-05-2024.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kwa cheo cha Dereva Daraja la II kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 25/05/2024 hadi 27/05/2024 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili
huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

  • Usaili utafanyika kuanzia tarehe 25/05/2024 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili. Muda wa kuanza usaili utakuwa saa moja kamili asubuhi (1:00 asubuhi) na sehemu ambapo usaili utafanyikia ni Ukumbi wa TRC Mwanga.
  • Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
  • Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, leseni ya udereva, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Barua ya Utambulisho kutoka ofisi za
    serikali ya kijiji/mtaa au Hati ya kusafiria.
  • Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI,
    Astashahada(Basic driving), Leseni ya Udereva na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji na viambatisho alivyoweka wakati anatuma maombi.
  • Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza
    matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA
    HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
  • Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
  • Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
  • Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na
    Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)

  • Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi
    vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
  • Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA MWANGA LEO MAY 18-2024

MAJINA 194 ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Mwanga 18-05-2024


CHIMBUKO/ASILI YA WILAYA YA MWANGA

  • Kihistoria tangu nyakati za Ukoloni, eneo la miinuko ya Kusini mwa Mlima Kilimanjaro na kati ya miinuko ya Usambara –Tanga pamoja na tambarare zake, na mgawanyo wa kiutawala uliitambua jina UPARE kama  neno la kutamkwa kama Wilaya ya Pare. Eneo hili lilikuwa na utawala wake wa wenyeji ambao tena ulitajwa kama Pare ya Kaskazini na Pare ya Kusini. Ambapo mwaka 1926 Chifu Kibacha Singo aliitisha machifu wote kwa lengo la kuunganisha wapare wote, hivyo mwaka 1928 wilaya ya Pare ilizaliwa
  • WILAYA YA PARE NA VIONGOZI WAKE 

Wilaya ya Pare ilikuwa inaongozwa na Machifu tisa (9) ambao kwa umoja wao walikuwa wanabadilishana uongozi kila baada ya mwaka mmoja.

Machifu hao ni kama ifuatavyo.

  1. SABUNI             NAGUVU                                   –        USANGI
  2. MINJA               KUKOME                                    –        UGWENO
  3. KIBACHA           SINGO                                       –        SAME
  4. MBWANA           YATERI (KIGHONO)                  –        GONJA
  5. DAUDI              SEKIMANGA    MANENTO          –        MAMBA
  6. YUSUFU            MAPOMBE                                 –        MBAGA
  7. CHAUKA            SAIDI      SADI                            –        HEDARU
  8. RUBENI             SHAZIA                                       –        SUJI
  9. IFOLONG’O        MAKANGE                                 –        CHOME/MAKANYA

Machifu hawa  walifanya kazi kwa kuzingatia matakwa ya wakoloni. Ili kuimarisha ulinzi katika eneo la hawa machifu palikuwa na walinzi waliokuwa wakiitwa Wachili, pamoja na kazi zao walihakikisha kuwa Chifu anakuwa katika hali ya usalama hivyo walipewa maeneo ya kuishi jirani na machifu. Kazi mojawapo ya Machifu ilikuwa ni kukusanya kodi  ( Poly Tax ).  Hata hivyo mnamo miaka ya hamsini machifu walishindwa kukidhi haja ya wakoloni hivyo chini yao wakaanzishwa Walao ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kukusanya kodi. Kwa kipindi hiki badala ya walao ni Makatibu Tarafa. Enzi za machifu palikuwa na Area  Commissioner (AC) ambao kwa namna nyingine waliitwa Bwana shauri kwani hao ndio walikuwa ni Mahakimu katika ngazi ya wilaya.

MAKABILA/LUGHA.

Wilaya ya Pare tangu zamani ilikuwa na wakazi wenye lugha mbili ( 2), kwa Pare zote za Kusini na Kaskazini lugha kuu ni Kipare. Kwa Pare ya Kaskazini na hususani maeneo ya Ugweno iko lugha kuu ya Kigweno, yenye lafudhi inayoendana zaidi na Kichagga kuliko Kipare.

WILAYA YA MWANGA. (1979 – MPAKA SASA).

Wilaya ya Mwanga ilianzishwa tarehe  1, Julai,1979 baada ya Uhuru wa Tanganyika, kwa hivi sasa  ni miongoni mwa wilaya Sita (6) za Mkoa wa Kilimanjaro, wilaya nyingine ni pamoja na Same, Rombo, Hai, Moshi na  Siha. Wakati wa kuanzishwa ilikuwa miongoni mwa wilaya  nne (4) ambazo zilikuwa Same, Moshi na Rombo, kabla ya kuanzishwa kwa wilaya mpya za Hai na Siha.

UTAWALA

Wakati wa kuanzishwa Wilaya ya Mwanga ilikuwa na Tarafa za Mwanga, Ugweno, Usangi na Lembeni kabla ya kuanzishwa Tarafa mpya ya Jipe Ndea. Wilaya ilikuwa na Kata  16,  Vijiji 53, na Jimbo moja la uchaguzi. Kwa sasa Wilaya  ina Tarafa 5 za Jipe Ndea, Mwanga, Lembeni, Usangi na Ugweno na ina Mamlaka ya Mji Mdogo 1 yenye Vitongoji 12. Wilaya ina Kata 19  za Mgagao, Lembeni, Kileo, Lang’ata, Kirya, Kivisini, Kwakoa, Toloha, Mwaniko, Kifula, Msangeni, Shighatini, Kighare, Chomvu, Ngujini, Kilomeni, Kigonigoni, Kirongwe  na  Jipe, kuna vijiji 72 na Vitongoji 272.

UKUBWA WA ENEO

Ukubwa wa eneo la Wilaya ni kilomita za mraba 2641 kati ya hizo eneo la ardhi ya nchi kavu ni  kilometa za mraba 2,558.6 na eneo la maji ni kilometa za mraba 82.4 ambapo Km 52 za mraba ni eneo la maji ya bwawa la Nyumba ya Mungu na Km 26.4 za mraba ni eneo la maji ya Ziwa Jipe.

WATU NA MAKAZI  

Wakati inaanzishwa Wilaya ya Mwanga mwaka 1979 ilikuwa na wakazi wapatao 74,620 na kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya 2022 Wilaya ilikuwa na idadi ya watu 148, 763, ambapo wanaume walikuwa 72,157, na wanawake walikuwa ni 76,606, na jumla ya kaya zilikuwa ni 38,847.

HALI  YA HEWA.

Wilaya  inapata mvua kati ya millimita 400- 600 kwa maeneo ya Nyanda za Chini na  kati ya millimita 800-1,200 kwa maeneo ya Nyanda ya Juu. Kuna misimu miwili ya mvua  Vuli na Masika. Vuli huanza mwezi Oktoba hadi Desemba na Masika huanza mwezi Machi hadi Juni. Maeneo ya Nyanda ya Juu hupata mvua zote za Vuli na Masika. Wilaya hupata upepo mkali unao vuma tokea upande wa  Mashariki kuelekea Magharibi, kiwango cha joto ni kati ya Nyuzi 14  sentigredi hadi Nyuzi  32 sentigredi hasa kwa mwezi Januari.

SHUGHULI ZA KIUCHUMI

1. KILIMO.

  • Wilaya ya Mwanga ni mojawapo ya wilaya ambazo zinapata mvua haba kila mwaka hivyo mazao yanayolimwa kwa kutegemea mvua hayana uhakika. Kwa wakazi wanaoishi milimani wanategemea kilimo cha ndizi, maharage kama mazao ya chakula na kahawa kama zao la biashara. Kwa miaka ya tisini uzalishaji wa zao la kahawa ulipungua sana kutokana na pembejeo kuwa ghali mno. Wakulima wa kahawa walianzisha chama cha ushirika VUASU ili kuimarisha soko la biashara. Zao la kahawa ndilo liliwasaidia sehemu ya wakazi wa Mwanga kusomesha watoto.

Kwa upande wa tambarare ya Mashariki na Magharibi kuna kilimo cha umwagiliji ambapo zao maarufu ni mahindi na mpunga kwa ajili ya biashara.

Asilimia 85 ya wananchi wanaishi vijijini.  Uchumi wa wilaya unategemea sana kilimo, ufugaji, uvuvi na sehemu ndogo wanajishughulisha na biashara ndogo ndogo.  Mazao makubwa ya biashara yanayolimwa ni Kahawa,na Mkonge . Mazao ya chakula ni Mahindi, Maharage, Ndizi, Mihogo, Viazi vitamu na Mpunga.

2. UFUGAJI.

Ufugaji unakwenda sambamba na kilimo kwani unachangia Wananchi kuinua kipato chao.  Kwa takwimu za mwaka 2016/17 Wilaya ina idadi ya Ng’ombe 117,007 wa kisasa wakiwa 14, 398 na kienyeji wakiwa 102, 609, Mbuzi 151,109, Kondoo 67, 102, Nguruwe 616, Sungura 196, Kuku 252 200, na  Bata 2, 340, Punda 1, 317, Ngamia 8. Mifugo hii huuzwa kwa ajili ya kujipatia kipato. Pia Ng’ombe hutoa maziwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kuuza ili kupata fedha za kujikimu kimaisha, na ngozi huuzwa katika masoko ya ngozi ndani na nje ya Wilaya na kuongeza mapato ya Wafugaji.

3. UVUVI.

Kuna shughuli  za Uvuvi katika Bwawa la Nyumba ya Mungu ambao ulianza mwaka 1969 baada ya Bwawa kujengwa. Pia kuna shughuli za uvuvi katika Ziwa Jipe  ambapo wavuvi pamoja na wananchi katika maeneo hayo hujipatia mapato kutokana na uvuvi na biashara ya uvuvi. Samaki wanaovuliwa huuzwa ndani na nje ya Wilaya ya Mwanga.

4. BIASHARA.

Wilaya ina  idadi ya biashara zifuatazo:- Baa na ‘’Grocery’’160, Maduka ya rejareja na Vioski 520,  Maduka ya jumla 3, Mikahawa 80, Gereji 5 ,Hotel 1, Motel 6,  Nyumba za kulala wageni 18, na kuna Vituo vya Mafuta  4 vinavyofanya kazi, na maduka ya hardware 14.

5. UFINYANZI.

  • Pamoja na kilimo wakazi wa wilaya ya Mwanga tangu hapo awali walijikita katika biashara ya kutengeneza vyungu hasa akina mama wa Usangi na kuviuza Moshi na Arusha hata Mombasa.

UONGOZI WA WILAYA YA MWANGA BAADA YA UHURU

Baada ya kuondolewa kwa utawala wa Machifu mwaka 1963, uongozi wa kiwilaya uliwekwa chini ya Wakuu wa Wilaya. Wakuu wa Wilaya (Area Commissioner) katika Wilaya ya Pare toka mwaka 1962 hadi 1979 walikuwa  wafuatao:-

Na.

Jina la Wakuu wa Wilaya

Muda

1

BWANA AMSIRONG ( MZUNGU)

1962

2

KAUGAHUA

1962 – 1963

3

MBWANA KIHERE

1963 – 1965

4

J. GWAHU

1965 – 1967

5

MADENGE

1967 – 1969

6

RWECHUNGURA

1969 – 1972

7 NYEMELE

1972 – 1975

8 MWAKATOBE

1975 – 1979

 

 ORODHA YA WAKUU WA WILAYA TOKA WILAYA YA MWANGA ILIPOANZISHWA MWAKA 1979

  

NA.

JINA KAMILI

MWAKA ALIOANZA

MWAKA ALIO ONDOKA

1 Bi Salome Philemoni  Nyiti

1979

1980

2 Bw.  Adolfu Abeli Mwakyusa

1980

1981

3 Bw. Pius Mkongoti

1981

1986

4 Bw. B. K. Sanga

1986

1992

5 Capt. T. L.A. Mwabeza

1992

1997

6 Bw. John  Tuppa

1997

2001

7 Bw. Rubeni  Ole – Kuney

2001

2005

8 Bw. Jordan O. Rugimbana

2005

2009

9 Bw. Athumani  Hassani  Mdoe

2009

2011

10 Shaibu I. Ndemanga

2012

2016

11 Aaron Y. Mbogho

2016

2019

12 Thomas Cornel Apson

2019

2021

13 Abdallah Mussa Mwaipaya

2021

Mpaka sasa

Tags: , , ,

Comments are closed.