NAFASI 4 za Kazi Wilaya ya Nyang’hwale July 10-2024
NAFASI 4 za Kazi Wilaya ya Nyang’hwale July 10-2024
NAFASI 4 za Kazi Wilaya ya Nyang’hwale July 10-2024, Nafasi 2 za Mwandishi Mwendesha Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale July 10-2024, Nafasi 2 za Msaidizi wa Kumbukumbu Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale July 10-2024, Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale 10-07-2024.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang`hwale amepokea kibali cha Ajira mpya kutoka kwa Katibu Mkuu OR – Utumishi chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024.
Hivyo anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa kada mbili (02) kama zilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa: –
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (“Office Management Secretary II” NAFASI 02)
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa Wahitimu wa kidato cha Nne au sita wenye Stashahada(Diploma) ya
Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya uhazili. Aidha ,wawe wamefaulu somo la
Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata
programu za kompyuta za ofisi kama vile:Word,Excel ,Powerpoint ,internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II.
- Kuchapa barua,taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.
- Kupokea wageni na kuwasaili shida zao , na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
- Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio ,miadi, wageni ,tarehe za vikao,safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine.
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
- Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika.
- Kukusanya ,kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali na
viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali- TGS C
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II (“Records Management Assistant II”NAFASI 02)
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Elimu ya kidato cha Nne (Form IV) au cha sita (Form VI) aliehitimu
mafunzo ya Stashahada /Diploma (NTA level 6) katika fani ya Masijala kutoka
vyuo vinavyotambuliwa na Serikali ,wenye ujuzi wa kompyuta.
KAZI NA MAJUKUMU YAMSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II.
- Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista (incoming
correspondence register) - Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi kwenye rejista (outgoing
correspondence register) - Kusambaza, majalada kwa watendaji (action officers)
- Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji.
- Kutafuta kumbukumbu /nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji;
- Kurudisha majalada kwenye kabati la majalada (racks/filing cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa;
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi(file tracking)
- Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali- TGS C
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipo kuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira Ulemavu
walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma. - Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E-mail Adress) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa
kuaminika. - Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo. - Maombi yote yaambatane na vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
kuzingatia sifa za kazi husika
Postgraduate/Degree/Advanced
Diploma/Diploma/Certificate – Cheti cha Mtihani wa Kidato cha nne na
cha Sita, Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Proffessional
Certificate from Respective Boards). - Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)BHAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na Vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo
katika Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010. - Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 22 Julai, 2024.
MUHIMU: kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –
Mkurugenzi Mtendaji ,
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 352,
NYANG`HWALE
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani
hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretariet ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulio ainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
DONWLOAD PDF DOCUMENT
POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 2 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale More Details |
2024-07-22 Login to Apply |
POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 2 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale More Details |
2024-07-22 Login to Apply |
Tags: Nafasi 2 za Msaidizi wa Kumbukumbu Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale July 10-2024, Nafasi 2 za Mwandishi Mwendesha Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale July 10-2024, NAFASI 4 za Kazi Wilaya ya Nyang'hwale July 10-2024, Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya wilaya ya Nyang'hwale 10-07-2024.