RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Kazi Hospital ya Sumbawanga January 19-2024

Filed in Ajira, Michezo by on 20/01/2024

NAFASI za Kazi Hospital ya Sumbawanga January 19-2024

NAFASI za Kazi Hospital ya Sumbawanga January 19-2024, Nafasi za Kazi za Kujitolea Hospital ya Sumbawanga January 19-2024,NAFASI za Kazi Hospital ya Sumbawanga January 19-2024, Walioitwa kazini sumbawanga manispaa, Sumbawanga Municipal Council.

NAFASI za Kazi Hospital ya Sumbawanga January 19-2024

NAFASI za Kazi Hospital ya Sumbawanga January 19-2024, Nafasi za Kazi za Kujitolea Hospital ya Sumbawanga January 19-2024,NAFASI za Kazi Hospital ya Sumbawanga January 19-2024, Walioitwa kazini sumbawanga manispaa, Sumbawanga Municipal Council.

Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga anakaribisha maombi ya kazi ya kujitolea kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo kama zilivyoanishwa katika Tangazo hili kama ifyatavyo;

WASAIDIZI WA HESABU DARAJA LA I (ACCOUNTS ASSISTANT I)
NAFASI (4)

KITUO CHA KAZI: Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga

MASHARTI YA AJIRA: – Mkataba wa kujitolea,

SIFA ZA MWOMBAJI

Mwombaji awe na sifa zifuatazo

  • Awe na Stashahada ya Uhasibu kutoka chuo kinachotambulika na Serikali AU
  • Awe na Cheti cha ATEC kinachotolewa na NBAA au sifa nyingine zinazolingana na hizo zinazotambulika na NBAA.

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuandika na kutunza “register” zinazohusu shughuli za uhasibu Kutunza kumbukumbu za hesabu.
  • Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu Benki.
  • Kutoa namba za malipo (Control Number) kwa wateja.
  • Kupendekeza na kuzuia mianya yote ya upotevu wa mapato ya Hospitali.
  • Kufanya kazi nyingine za fani yake atakakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

MSHAHARA NA STAHIKI NYINGINE

Malipo ya mshahara yatazingatia mwongozo wa Taifa wa kujitolea wa Julai, 2021 (National Health Workers Volunteering Guideline).

Aidha malipo mengine yataendelea kulipwa kwa kuzingatia miongozo mbalimbali iliyopo ya Serikali

DAKTARI (MEDICAL DOCTOR)

NAFASI (1)

KITUO CHA KAZI: Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga

MASHARTI YA AJIRA: Mkataba wa kujitolea

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Waombaji wawe na Shahada ya Udaktari kutoka Chuo kinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza “Internship” na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).
  • MAJUKUMU YA KAZI.Kuhakikisha fomu za Bima ya Afya zinajazwa kwa usahihi na kikamilifu.
  • Kuwaona Wagonjwa katika “Clinic’ya Bima ya Afya, kufanya kazi za matibabu hospitalini zinazohusiana na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya watoto, magonjwa ya akina Mama, upasuaji wa kawaida na dharura.
  • Kufuatilia makato ya malipo ya Bima ya Afya.
  • Kufanya maboresho ya ujazaji wa fomu za Bima ya Afya.
  • Kuongeza Ufanisi na tija katika ukusanyaji wa mapato yanayotokana na uchangiaji wa huduma za afya( malipo ya papo kwa papo na Bima mbalimbali za Afya.
  • Kufundisha wanafunzi wa vyuo vya Afya.
  • Kushiriki katika Kutengeneza na kusimamia utekelezaji wa sera za Serikali kuhusu Afya yako.
  • Kuandaa mipango na makisio ya bajeti ya huduma za Afya.
  • Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma katika fani.
  • Kufanya kazi nyingine utakazopangiwa na Mkuu/ Msimamizi wako wa kazi zinazohusiana na Elimu, Uzoefu na Ujuzi wako.

MSHAHARA NA STAHIKI NYINGINE

  • Malipo ya mshahara yatazingatia mwongozo wa Taifa wa kujitolea wa Julai, 2021 (National Health Workers Volunteering Guideline).
  • Aidha malipo mengine yataendelea kulipwa kwa kuzingatia miongozo mbalimbali iliyopo ya Serikali.

MTEKNOLOJIA DAWA DARAJA LA II.
NAFASI (1)

KITUO CHA KAZI: Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga

MASHARTI YA AJIRA: Mkataba wa Kujitolea

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Mwombaji awe na Stashahada ya Famasi (Diploma in Pharmaceutical Science) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali na lazima awe na usajili kamili na hai kutoka Baraza la Famasi.

NAFASI za Kazi Hospital ya Sumbawanga January 19-2024, Nafasi za Kazi za Kujitolea Hospital ya Sumbawanga January 19-2024,NAFASI za Kazi Hospital ya Sumbawanga January 19-2024, Walioitwa kazini sumbawanga manispaa, Sumbawanga Municipal Council.MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuainisha,kuandaa na kuagiza mahitaji ya dawa na vifaa tiba katika eneo lake la kazi.
  • Kugawa dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa na watumishi.
    Kuchanganya dawa.
  • Kuhifadhi dawa na vifaa tiba.
    Kuelimisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya dawa.
  • Kukagua dawa,vifaa tiba kemikali,vitendanishi na vipodozi katika eneo lake la kazi.
  • Kutoa taarifa juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya dawa. Kuratibu kazi za kamati ya dawa ya hospitali.
  • Kuandaa taarifa ya matumizi ya dawa na vifaa tiba.
  • Kufanya uchunguzi wa ubora wa dawa,vifaa tiba kemikali, vitendanishi na vipodozi,
  • Kufanya kaguzi mbalimbali katika sehemu zinazohifadhi dawa.
  • Kutunza kumbukumbu za dawa na vifaa tiba.
  • Kufanya kazi nyingine utakazopangiwa na mkuu wako wa kazi zinazohusiana na elimu,uzoefu na ujuzi wako.

MSHAHARA NA STAHIKI NYINGINE

  • Malipo ya mshahara yatazingatia mwongozo wa Taifa wa kujitolea wa Julai, 2021 (National Health Workers Volunteering Guideline).
  • Aidha malipo mengine yataendelea kulipwa kwa kuzingatia miongozo mbalimbali iliyopo ya Serikali

WAHUDUMU WA AFYA (HEALTH ASSISTANTS)

NAFASI (4)

KITUO CHA KAZI: Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga

MASHARTI YA AJIRA: Mkataba wa Kujitolea

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Mwombaji awe amehitimu kidato cha nne waliopata mafunzo ya mwaka mmoja katika fani ya Afya.

MAJUKUMU YA KAZI.

  • Kufanya kazi ya kuwaongoza wagonjwa katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma (eneo la kujiandikishia,vyumba vya madaktari,sehemu za vipimo kama Maabara na Idara ya mionzi na Maeneo mengine kadiri ya uhitaji wa huduma kwa mteja.
  • Kufuatilia mahitaji ya dawa kwa wagonjwa kutka hifadhi ya dawa.
  • Kuchukua sampuli za mgonjwa kwaajili ya vipimo vya maabara na kufuatilia majibu.
  • Kusaidia wagonjwa wasiojiweza na walemavu kwenda sehemu mbalimbali za kutolea huduma.
  • Kufanya shughuli nyingine utakazopangiwa na kiongozi wako wa kazi.

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE

Waombaji wote wawe raia wa Tanzania wasiozidi umri wa miaka 45

Waombaji wawasilishe barua ya maombi na nakala zifuatazo.

Sifa binafsi (CV)

  • Cheti cha kuzaliwa.
  • Kitambulisho cha taifa (NIDA) au namba za kitambulisho
  • Vyeti vya elimu ya Sekondari (Kidato cha nne na sita kulinga na fani husika)
  • Vyeti vya taalumu katifa fani husika
  • Usajili (Full Registration) Kitaaluma kwa kada zilizo chini ya Mabaraza ya Kitaaluma.
  • Vyeti vilivyotolewa na Bodi za mitihani za nje ya Tanzania vya elimu ya kidato cha nne (CSE) au elimu ya Kidato cha sita (ACSE) vinapaswa kuthibitishwa na Baraza la Mitihani ya Taifa la Tanzania (NECTA)
  • Aidha vyeti vilivyotolewa na vyuo vikuu vya nje ya Tanzania vilivyothibitishwa na Tume ya vyuo vikuu nchini (TCU) Vitapokelewa.
  • Barua za maombi ziwasilishwe kwa lugha ya kiswahili/ kingereza.

JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI

Maombi yote yawasilishwe kufikia au kabla ya tarehe 11 Februari, 2024 kwa njia ya EMS/ Kwa mkono Ofisi ya Masjala ya wazi iliyopo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga.

Barua zinapaswa kuandikwa kwa;
Mganga Mfawidhi,
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa,
S.L.P. 413,
SUMBAWANGA.

NB: Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga haitahitaji waombaji kutoa fedha/kitu chochote katika hatua zote za ajira hizi za Mkataba.

NAFASI za Kazi Hospital ya Sumbawanga January 19-2024 DOWNLOAD PDF

Kuitwa kwenye usaili halmashauri, Nafasi za kazi Sumbawanga 2024, Ajira portal, Sekretarieti ya ajira, AJIRA LEO, Sumbawanga vijijini, Mkuu wa wilaya sumbawanga, Ramani ya sumbawanga mjini, Mitaa ya sumbawanga mjini,
Shule za sekondari sumbawanga vijijini, Nijuze Habari Ajira Portal.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Tags: , , ,

Comments are closed.