RASMI Prince Mpumelelo Dube ni Mwananchi
RASMI Prince Mpumelelo Dube ni Mwananchi
RASMI Prince Mpumelelo Dube ni Mwananchi,Klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa Mshambuliaji, Prince Mpumelelo Dube kwa mkataba wa miaka miwili.
Dube ambaye ana uzoefu wa soka la Bongo akicheza kwa miaka minne ndani ya Azam FC, anaingia katika kikosi Cha Young Africans kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji.
Nyota huyo raia wa Zimbabwe, ni mzuri katika kufunga magoli na kutengeneza nafasi za kufunga akiwa na uwezo mkubwa wa kusimama kama
Mshambuliaji wa mwisho na kutokea pembeni upande wa kushoto na kulia.
Katika misimu minne aliyokuwa akiitumikia Azam akitokea Highlanders FC ya kwao Zimbabwe, Dube
amefanikiwa kufunga magoli 34 ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara pekee.
Ubora wa Dube haujifichi kwani amekuwa mchezaji wa kuamua
matokeo katika mechi kubwa kutokana na kufunga magoli muhimu.
Usajili wa Dube unadhihirisha wazi kwamba Klabu hiyo inaimarisha zaidi kikosi chao kuelekea msimu ujao wa 2024)2025 ambapo malengo makubwa ni kutetea mataji yao yote ya 2023/2024 ambayo ni Ligi Kuu ya NBC na Kombe la Shirikisho la CRDB Bank.
Pia malengo mengine ya Yanga ni kubeba Ngao ya Jamii na kufika mbali Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya msimu uliopita 2023-2024 kuishia robo fainali.
Usajili Dune unakuwa usajili wa pili baada ya kukamilisha usajili wa, Clatous Chama July 01-2024, huku pia Klabu hiyo ikifanikiwa kuwaongezea mikataba Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery, Nickson Kibabage na Bakari Nondo Mwamnyeto.