RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


TETESI Za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025

Filed in Usajili, Michezo by on 20/06/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

TETESI Za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025

TETESI Za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025, TETESI Za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara Dirisha Dogo la Usajili 2024/2025, Usajili Simba, Usajili Yanga, Usajili Azam.

Klabu ya Pamba Jiji Fc imethibitisha kuachana na wachezaji wote pamoja na benchi lote la ufundi ambao waliipandisha timu daraja wakidai kumalizika kwa mikataba yao wote klabuni hapo.

Pamba Jiji FC ambayo imepanda Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara msimu ujao wa 2024/2025 ipo kwenye mchakato wa kutengeneza timu mpya kwaajili ya msimu huo.

Samson Madeleka amejiunga na Pamba Jiji akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na klabu ya Mashuja kutamatika.

Madeleka àlijiunga na Mashujaa akitokea Mbeya City

Baada ya kuachana na Pamba Jiji Mbwana Makata yupo mbioni kujiunga na Tanzania Prisons kuwa kocha mkuu wa timu hiyo

Makata anaenda kuchukuwa nafasi ya kocha Ahmad Ally

Coastal Union ipo Kwenye mazungumzo na mshambuliaji, Maulid Shaban ambaye ni mchezaji huru Kwa Sasa baada ya mkataba wake kutamatika ndani ya klabu ya Mbeya City mwishoni mwa msimu uliopita.

Katika msimu uliopita alifunga mabao 17 na kutoa pasi za mabao (Assist) 7.

Beki wa kushoto Aboubakar Mfaume Ngelema ni mchezaji huru baada ya mkataba wake kuisha mwishoni mwa msimu uliopita ndani ya Dodoma Jiji

Mshambuliaji Ibrahim, Ali Mkoko huenda akajiunga na Dodoma Jiji (mazungumzo yanaendelea)

Ali Mkoko na klabu yake ya Namungo hakuna mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya baada ya mkataba wa awali kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita.

Mkataba wa mwanadada, Edna Lema umemalizika ndani ya klabu ya Biashara Utd ambapo alikuwa kocha msaidizi wa timu hiyo.

Kuna uwezekano mkubwa wa mwanadada huyo maarufu Kwa jina la Mourinho kurudi kuifundisha timu ya wanawake ya Yanga princess

Kuna uwezekano mkubwa wa aliekuwa kocha wa Tz Prisons, Ahmad Ally kuwa kocha wa JKT Tz akichukuwa mikoba ya Malale Hamsini Kea

Baada ya kudumu Kwa takribani miaka 7, Sadala Mohamed Lipangile amechana na klabu yake ya KMC

Sadala alijiunga na KMC mwaka 2017 akitokea Mbao Fc

Baada ya kuwafungashia vilago bechi lote la ufundi klabu ya Mtibwa Sugar huenda ikamkabidhi Awadhi Juma kuwa kocha wao mkuu katika msimu ujao wa kujitafta kurudi ligi Kuu

David Luende aliyejiunga na Kagera Sugar mwaka 2018 amemaliza mkataba wake na timu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita.

hadi jana hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika juu ya kuongeza mkataba mpya.

George Makang’a ni mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika ndani ya KMC mwishoni mwa msimu uliopita.

Makang’a amewahi kuvitumikia vilabu vya Biashara Utd, Namungo Fc na Mtibwa Sugar na alijiunga na KMC akitokea Mtibwa Sugar miaka miwili 2 iliyopita.

Klabu Ya Geita Gold imeulizia huduma ya kocha mkuu wa Kagera Sugar Felix Minziro kuwa kocha wao mkuu

Mazungumzo bado hayajawa chanya.

Kagera Sugar wanamtafta Melis Medo kuwa mrithi wa Minziro, endapo ataondoka klabuni hapo.

Masoud Abdallah ameachana rasmi na klabu yake ya KMC

Masoud alijiunga na KMC akitokea Azam Fc miaka 3 iliyopita

Mk14 ni mchazaji huru baada ya mkataba wake na Singida FG kutamatika mwishoni mwa msimu uliopita.

Kagere alikuwa Namungo Kwa mkopo wa miezi 6 hivyo mkataba wake wa mkopo umemalizika ndani klabu ya Namungo na hatoendelea nao

Beki wa kati, Justine Omery ni mchezaji huru baada kumaliza mkataba wake wa miaka 2 ndani ya klabu ya Dodoma Jiji

Azam Fc wamefanikiwa kuinasa saini ya golikipa wao Mohamed Mstapha Kwa mkataba wa kudumu.

Awali nyanda huyo alikuwa anaitumikia Kwa mkopo akitokea El Merreikh

Golikipa Muhammed Hussein Mohamed “Muddy Colour” amefikia makubaliano ya kuongeza mkataba mpya wa miaka 2 wa kuendelea kuwa mlinda lango wa klabu ya Dodoma Jiji

Makubaliano kati ya Dodoma Jiji na golikipa huyo tayari yalishafikiwa, kinachosubiliwa ni Muddy kwenda Dodoma Kwa ajili ya kusaini rasmi.

Aliyekuwa Mshambuliaji wa klabu ya KMC, Waziri Jr ameshafikia makubaliano binafsi na klabu ya Singida Black Stars

Mkataba uliozungumziwa ni wa miaka 2 ila bado hajasaini rasmi Singida Black Stars

KMC wanahaha kumubakisha baada ya mkataba wake kutamatika mwishoni mwa msimu uliopita hivyo Kwa sasa Waziri Jr bado ni mchezaji huru

Edna Lema atasaini mkataba amefikia makubaliano ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuwa kocha mkuu wa Yanga princess

Kocha huyo maarufu Kwa jina la Mourinho alikuwa kocha msaidizi wa klabu ya Biashara Utd ya mkoani mara hivyo amejiunga na Yanga Princess baada ya mkataba wake na Biashara Utd kutamatika

Ikumbukwe Edna Lema aliwahi kuwa kocha mkuu wa Yanga princess

Mshambuliaji Ismail Mgunda amejiunga na Mashujaa Fc ya mkoani kigoma Kwa mkataba wa mwaka mmoja akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Singida Black Stars zamani Ihefu fc kufikia tamati mwishoni mwa msimu uliopita.

Mgunda alijiunga na Singida Black Stars zamani Ihefu fc akitokea Tanzania Prisons mwaka Jana mwezi July

Klabu ya Pamba Jiji imeachana rasmi na Jamal Mtegeta baada ya mkataba wake kutamatika

Mtegeta alijiunga na Pamba Jiji Kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Dodoma Jiji mwaka jina mwezi Juni

Kagera Sugar tayari imeanza mazungumzo ya kumuongeza mkataba mpya kocha wake Felix Minziro

Hadi sasa hakuna makubaliano yaliyofikiwa

Mtanzania Murshid Ally Kika amepewa kazi ya kocha wa viungo katika klabu ya El Merreikh ya Sudani

El Merreikh ipo nchini Tz Kwaajili ya kujiandaa na msimu ujao huku ukisubili kucheza michuank Kagame Cup

Klabu ya Dodoma Jiji imemtambulisha rasmi kocha wao mpya Meck Mexime akichukuwa mikoba ya Francis Baraza alieondoka baada ya mkataba wake kutamatika mwishoni mwa msimu uliopita

Meck amejiunga na Dodoma Jiji akiwa kocha huru baada ya mkataba wake kutamatika mwishoni mwa msimu uliopita ndani ya klabu ya Singida Black Stars zamani Ihefu Fc

Thabang Sesinyi Coastal Union FC

Thabang Sesinyi Coastal Union FC

Klabu ya Coastal Union imeanza mazungumzo ya kumsajili winga wa Jwaneng Galaxy ya Botswana, Thabang Sesinyi ili kuongeza nguvu msimu ujao hasa kwa Kombe la Shirikisho Afrika.

Augustine Okrah Bechem United

Augustine Okrah Bechem United

Klabu ya Bechem United ya Ghana imepanga kumrejesha winga wa Young Africans, Augustine Okrah aliyeonekana kutokuwa kwenye mipango ya kocha Miguel Gamondi.

Khomeiny Aboubakar Young Africans

Khomeiny Aboubakar Young Africans

Klabu Young Africans imeanza mazungumzo na Singida Black Stars kwaajili ya kumpata kipa wa timu hiyo, Khomeiny Aboubakar endapo itamkosa Yona Amos wa Tanzania Prisons.

Wazir Junior KMC FC

Wazir Junior KMC FC

Klabu ya Azam FC imeanzisha mazungumzo na Mshambuliaji wa KMC FC, Wazir Junior kuona kama watafikia makubaliano ya kupata saini yake kwaajili ya msimu ujao wa 2024/2025.

Damaro Camara Simba SC

Damaro Camara Simba SC

Klabu ya Simba imeanza mazungumzo ya kuinasa Saini ya kiungo mkabaji anayeweza kucheza kama beki wa kati, Damaro Camara mwenye umri wa miaka 20 kutoka Hafia ya kwao Guinea.

Juma Mgunda Coastal Union FC

Juma Mgunda Coastal Union FC

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda anadaiwa kuwa mbioni kurejea Coastal Union kwa nia ya kwenda kuiongezea nguvu timu hiyo ambayo ipo chini ya David Ouma ikijiandaa kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Lumiere Banza Kalumba Tabora United FC

Lumiere Banza Kalumba Tabora United FC

Klabu ya Coastal Union imeanza mazungumzo ya kumpata Mshambuliaji wa Tabora United FC, Lumiere Banza Kalumba raia wa DR Congo kwaajili ya msimu ujao.

Rahim Shomary Simba SC

Rahim Shomary Simba SC

Uongozi wa Simba umeanzisha mazungumzo ya kumpata beki wa kushoto wa KMC FC, Rahim Shomary mwenye umri wa miaka 19 kwaajili ya kuiongezea nguvu timu hiyo Kuelekea Msimu Mpya wa 2024/2025.

Ramadhan Salum Chobwedo TMA FC

Ramadhan Salum Chobwedo TMA FC

Klabu ya Tanzania Prisons, imeanza hesabu za kuinasa saini ya Mshambuliaji wa TMA FC, Ramadhan Salum Chobwedo kwaajili ya msimu ujao wa 2024/2025.

Denis Nkane Mashujaa FC, Pamba Jiji & Ken Gold

Denis Nkane Mashujaa FC, Pamba Jiji & Ken Gold

Klabu za Mashujaa FC, Pamba Jiji na Ken Gold zimetajwa kumnyemelea winga wa Yanga, Denis Nkane kwaajili ya kuimarisha vikosi vyao Kuelekea Msimu Mpya wa 2024/2025.

Joshua Mutale Simba SC

Joshua Mutale Simba SC

Klabu ya Simba ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa winga, Joshua Mutale mwenye umri wa miaka 22 kutoka Power Dynamos ya kwao Zambia.

Nassoro Kapama Mtibwa Sugar

Nassoro Kapama Mtibwa Sugar

Klabu za Dodoma Jiji, Mashujaa na JKT Tanzania zinapigana vikumbo kuiwania saini ya Nassoro Kapama ambaye amemaliza mkataba wake wa miezi sita na Mtibwa Sugar iliyoshuka daraja.

Juma Nyangi Mtibwa Sugar

Juma Nyangi Mtibwa Sugar

Klabu za Kagera Sugar, KMC FC, Coastal Union na Dodoma Jiji, zimeonyesha nia ya kuhitaji saini ya kiungo wa Mtibwa Sugar iliyoshuka daraja, Juma Nyangi.

Andy Bikoko Tabora United

Andy Bikoko Tabora United

Klabu za Singida Fountain Gate, Pamba Jiji na Singida Black Stars zimeingia Katika vita ya kuwania saini ya beki wa Tabora United, Andy Bikoko raia wa DR Congo.

Anita Adongo Alliance Girls

Anita Adongo Alliance Girls

Klabu za Simba Queens na Yanga Princess zimeingia kwenye vita ya kumuwinda beki wa kati wa Alliance Girls, Anita Adongo ambaye anamaliza mkataba mwishoni mwa msimu huu.

Nelly Kache Alliance Girls

Nelly Kache Alliance Girls

Klabu ya Ceasiaa Queens inatajwa kuwa miongoni mwa timu zinazohitaji huduma ya Kiungo wa Alliance Girls, Nelly Kache.

Valentin Nouma Simba SC

Valentin Nouma Simba SC

Klabu ya Simba inatajwa kuwa kwenye mazungumzo na beki wa kushoto wa FC Saint Eloi Lupopo ya DR Congo, Valentin Nouma raia wa Burkina Faso mwenye umri wa miaka 24 kwaajili ya kuipata huduma yake Kuelekea Msimu Mpya wa 2024/2025.

Joyce Lomalisa Simba SC

Joyce Lomalisa Simba SC

Jean Othos Baleke Azam FC & Young Africans

Jean Othos Baleke Azam FC & Young Africans

Aliyekuwa Mshambuliaji wa Simba, Mkongomani, Jean Othos Baleke yupo nchini akiwa katika mazungumzo na timu mbili ambazo ni Azam FC na Young Africans

Inaelezwa kuwa Baleke aliyecheza Simba kwa mkopo akitokea TP Mazembe ya kwao DR Congo kabla ya kutimkia Al Ittihad ya Libya mwaka huu, yupo nchini kwaajili ya kukamilisha usajili wa kujiunga na kati ya Azam FC au Young Africans.

Edgar Wiliams Kengold FC

Edgar Wiliams Kengold FC

Klabu ya Pamba Jiji ya Jijini Mwanza iliyopanda Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2024/2025 inaendelea kuboresha kikosi chake na sasa imetua kwa Mshambuliaji wa Ken Gold, Edgar Wiliams aliyeibuka kinara wa ufungaji kwenye Championship.

Victorien Adebayo & Mohamed Kamara Singida Black Stars FC

Victorien Adebayo & Mohamed Kamara Singida Black Stars FC

Klabu ya Singida Black Stars inadaiwa kuwa kwenye mazungumzo na Mshambuliaji Victorien Adebayo kutoka AS GNN ya kwako Nigeria pamoja na golikipa, Mohamed Kamara kutoka AC Horoya ya Guinea.

Adebayor aliyewahi kucheza RS Berkane na AmaZulu kabla ya kurejea kwao Niger anaitajika haraka ili kuziba nafasi ya Emmanuel Bola Labota anayetakiwa Young Africans.

Ayoub Lyanga Azam FC

Ayoub Lyanga Azam FC

Klabu ya Azam FC imedaiwa kuwa kwenye hatua nzuri ya kumuongezea mkataba mpya winga wake, Ayoub Lyanga ili asalie kikosini hapo.

Aboutwalib Mshery Young Africans

Aboutwalib Mshery Young Africans

Golikipa wa Klabu ya Yanga, Aboutwalib Mshery amemaliza mkataba wake na Klabu hiyo, wakati akisubiria hatma yake klabu ya Azam imetajwa Kuanza Mazungumzo naye.

Edward Charles Manyama Al Hilal Sudan

Edward Charles Manyama Al Hilal Sudan

Baada ya kumaliza mkataba wa kuitumikia Azam FC, beki Edward Charles Manyama ametajwa kuwaniwa Al Hilal ya Sudan na muda wowote anatatajiwa Kusaini Mkataba Mpya.

Klabu ya Dodoma Jiji imetajwa kuwa Katika hatua za mwisho kumsajili, Meck Mexime kwaajili ya kuchukuwa nafasi ya Francis Baraza aliyeachana na timu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika

Mexime atajiunga na Dodoma Jiji baada ya kuachana na Singida Black Stars zamani Ihefu Fc.

Involata Mukoshi Fountain Gate Princess

Involata Mukoshi Fountain Gate Princess

Klabu za Simba Queens, Yanga Princess pamoja na Police Bullets ya Kenya zimepiga hodi kunako Fountain Gate Princess kuiwania saini ya kiungo Mkenya Involata Mukoshi ambaye anamaliza mkataba Msimu huu.

Athuman Masumbuko Mashujaa FC

Athuman Masumbuko Mashujaa FC

Mshambuliaji wa Mashujaa FC, Athuman Masumbuko amepanga kuachana na timu hiyo baada ya kutokuwa na msimu mzuri msimu ulioisha wa 2023/2024.

Najim Mussa Tabora United

Najim Mussa Tabora United

Uongozi wa Singida Black Stars umeingilia kati dili la kiungo wa Tabora United, Najim Mussa ambaye ametajwa kuwaniwa na timu mbalimbali zikiwemo za Simba SC na Azam FC.

Winifrida Gerald JKT Queens

Winifrida Gerald JKT Queens

Klabu ya Simba Queens imeanza mazungumzo ya kumnunua moja kwa moja winga wa JKT Queens, Winifrida Gerald anayemaliza mkataba mwishoni mwa mwezi huu.

Ian Otieno Zesco United

Ian Otieno Zesco United

Klabu ya Azam FC imeanza Mazungumzo na Klabu ya Zesco ya Zambia ili kuona uwezekano wa kumpata kipa, Ian Otieno kwaajili ya kuchukua nafasi ya Mohamed Mustafa aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka Al-Merrikh ya kwao Sudan ambaye hawana uhakika wa kusajilia klabuni hapo.

Hussein Masalanga Ihefu FC

Hussein Masalanga Ihefu FC

Golikipa Hussein Masalanga rasmi ameachana na Ihefu Fc baada ya mkataba wake kutamatika ndani ya klabu hiyo.

Saido Ntibanzokinza Simba SC

Saido Ntibanzokinza Simba SC

Kiungo wa klabu ya Simba SC, Saido Ntibanzokinza raia wa Burundi ameachana rasmi na Klabu hiyo.

Malickou Ndoye, Issah ndala, Ali Ahmada

Malickou Ndoye, Issah ndala, Ali Ahmada

Klabu ya Azam Fc imeachana na beki wake Malickou Ndoye, Azam pia inatarajiwa kuachana na Abdulai Idrisu, Issah ndala pamoja na Ali Ahmada.

Jonas Mkude, Kibwana Shomari, Bakari Nondo Mwamnyeto, Salum Abubakar

Jonas Mkude, Kibwana Shomari, Bakari Nondo Mwamnyeto, Salum Abubakar

Klabu ya Yanga sc imepanga kuwaongeza mikataba mipya wachezaji Salum Abubakar, Jonas Mkude, Bakari Nondo Mwamnyeto pamoja na Kibwana Shomari.

Cheikh Sidibe Azam FC

Cheikh Sidibe Azam FC

Mchezaji Cheikh Sidibe ameomba kuondoka ndani ya Klabu ya Azam Fc.

Mohamed Mustapha Azam FC

Mohamed Mustapha Azam FC

Golikipa wa klabu ya Azam FC, Mohamed Mustapha atarejea kwenye klabu yake ya Al Mereikh dirisha lijalo la Usajili baada ya mkopo wa miezi 6 kuisha.

Goran Kopunovic Pamba Jiji FC

Goran Kopunovic Pamba Jiji FC

Klabu ya Pamba Jiji iliyopanda Ligi Kuu ipo mbioni kumsajili aliyewahi kuwa Kocha wa Vilabu vya Simba SC na Tabora United, Goran Kopunovic.

Yusuph Kagoma Simba SC

Yusuph Kagoma Simba SC

Kiungo, Yusuph Kagoma yupo mbioni kujiunga na klabu Simba SC akiwa Mchezaji huru baada ya kuachana na Singida Fountain Gate FC.

Salum Athuman ‘Stopper’ Simba SC

Salum Athuman ‘Stopper’ Simba SC

Klabu ya Simba inajaribu kufanya mazungumzo ya kumsajili beki wa KVZ ya Zanzibar, Salum Athuman ‘Stopper’ ambaye amekuwa na kiwango bora.

Brian Mandela Onyango Simba SC

Brian Mandela Onyango Simba SC

Klabu ya Simba inamuwania beki wa kati wa Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini raia wa Kenya, Brian Mandela Onyango mwenye miaka 29.

Seif Abdallah Karihe Mashujaa FC

Seif Abdallah Karihe Mashujaa FC

Klabu ya Mashujaa FC imetajwa Kuanza Mazungumzo na aliyekuwa mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Seif Abdallah Karihe ili kuziba nafasi ya Adam Adam aliyerejea Azam FC.

Yannick Bangala Azam FC

Yannick Bangala Azam FC

Viongozi wa Simba wametajwa kufanya mawasiliano na wakala wa kiungo, Yannick Bangala anayeichezea Azam FC ili kuangalia uwezekano wa kumpata nyota huyo wa zamani ya Young Africans.

Farid Mussa Yanga SC

Farid Mussa Yanga SC

Klabu ya Azam FC imetajwa kuanza mazungumzo ya kumrejesha winga wa zamani wa timu hiyo, Farid Mussa aliyemaliza mkataba huko Young Africans.

Yona Amosi Tanzania Prisons FC

Yona Amosi Tanzania Prisons FC

Golikipa Yona Amosi yupo huru baada ya mkataba wake kumalizika ndani ya timu yake ya Tanzania Prisons FC.

Pa Omar Jobe Simba SC

Pa Omar Jobe Simba SC

Klabu ya Simba huenda ikaachana mshambuliaji wake, Pa Omar Jobe mazungumzo yanakaribia kukamilika.

Erick Johora Mashujaa FC

Erick Johora Mashujaa FC

Klabu ya Mashujaa ipo kwenye mazungumzo ya kumuongeza mkataba mpya golikipa wake, Erick Johora.

Kipa huyo wa zamani wa vilabu vya Eagle Noir na Yanga sc alijiunga na Mashujaa Kwa mkataba wa miezi 6 akitokea Geita Gold

Sebu Sebu Geita Gold

Sebu Sebu Geita Gold

Klabu ya Dodoma Jiji imetajwa kutuma ofa ya kuhitaji golikipa, Sebu Sebu baada mkataba wake kumalizika ndani ya klabu ya Geita Gold.

Geofrey Muha Geita Gold

Geofrey Muha Geita Gold

Vilabu vya KMC FC, Kengold, na Tanzania Prisons vinaiwania Saini ya beki Geofrey Muha baada ya mkataba wake na Geita Gold kumalizika.

Derrick Mukombozi Namungo FC

Derrick Mukombozi Namungo FC

Uongozi wa Simba SC upo kwenye mazungumza ya kunasa saini na beki wa Namungo na timu ya taifa ya Burundi, Derrick Mukombozi kwaajili ya kuziba pengo la Henock Inonga ambaye anatajwa kutaka kuondoka klabuni hapo.

Amina Bilal Yanga Princess

Amina Bilal Yanga Princess

Klabu ya Yanga Princess imeanza maandalizi mapema ya msimu ujao baada ya kumfuata kiungo wa JKT Queens, Amina Bilal ambaye mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu huu.

Deusdedith Okoyo Pamba Jiji FC

Deusdedith Okoyo Pamba Jiji FC

Kuna uwezekano mkubwa wa beki wa kushoto, Deusdedith Okoyo akajiunga na Pamba Jiji ya Jijini Mwanza iliyopanda daraja msimu huu.

Richaldson Ng'odya Kagera Sugar FC

Richaldson Ng’odya Kagera Sugar FC

Klabu ya JKT Tanzania imeanza hesabu za usajili wa winga wa Kagera Sugar FC, Richaldson Ng’odya.

Kenneth Semakula Simba SC

Kenneth Semakula Simba SC

Klabu ya Simba ipo kwenye mazungumzo na aliyekuwa kiungo wa SC Villa ya Uganda, Kenneth Semakula ili kujiunga nao msimu ujao.

Kennedy Juma Simba SC

Kennedy Juma Simba SC

Klabu ya Coastal Union imeanza hesabu za kumnasa beki wa Simba, Kennedy Juma baada ya mkataba wake kumalizika msimu huu.

Hiyo inatokana na kuondokewa na beki wa kikosi hicho, Lameck Lawi ambaye tayari msimu ujao atajiunga na Simba baada ya kufikia makubalino baina ya timu hizo na kusainishwa mkataba wa miaka miwili.

Austin Odhiambo Singida Black Stars

Austin Odhiambo Singida Black Stars

Klabu ya Singida Black Stars, inawania saini ya kiungo mshambuliaji wa Gor Mahia, Austin Odhiambo kwaajili ya kujiunga nao msimu ujao.

Taarifa zinaeleza nyota wawili wa Kenya, Elvis Rupia na Duke Abuya ndio ambao wanatumika kama chambo cha kumshawishi kiungo huyo japo changamoto kubwa inayoweza kutokea ni kutokana na Gor Mahia kufuzu Ligi ya Mabingwa.

Saidi Zanda Stand United FC

Saidi Zanda Stand United FC

Kiungo Mshambuliaji, Saidi Zanda yupo huru baada ya mkataba wake na klabu ya Stand United ya mkoani shinyanga inayoshiriki Championship kumalizika.

Hashimu Manyanya Namungo FC

Hashimu Manyanya Namungo FC

Baada ya kuitumikia Namungo Kwa takribani misimu mitano (5) mfululizo Hashimu Manyanya yupo huru baada ya mkataba wake kutamatika mwishoni mwa msimu uliopita.

Taarifa ambazo Nijuze Habari inazo hadi Sasa hakuna mazungumzo yaliyofanyika kuhusu kuongezewa mkataba mpya na klabu hiyo.

Yusuph Valentino Mhilu Kagera Sugar FC

Yusuph Valentino Mhilu Kagera Sugar FC

Yusuph Valentino Mhilu yupo huru baada ya mkataba wake na Geita Gold kutamatika tangu May 2024.

Muhilu amekulia Kwenye timu ya vijana ya Yanga Sc, pia amewahi itumukia Kagera Sugar Kwa nyakati tofauti

Eliud Ambokile Mbeya City

Eliud Ambokile Mbeya City

Mashambuliaji wa Zamani wa TP Mazembe ya DR Congo, Eliud Ambokile ni mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika ndani ya klabu ya Mbeya City inayoshiriki Championship.

Mohamedi Hussein Mudi Colour dodoma jiji

Mohamedi Hussein Mudi Colour dodoma jiji

Golikipa, Mohamedi Hussein maarufu kwa jina la Mudi Colour yupo huru baada kumaliza mkataba wake na Dodoma Jiji FC ya Dodoma.

Salum Kihimbwa Mtibwa Sugar

Salum Kihimbwa Mtibwa Sugar

Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Mtibwa Sugar, Dodoma Jiji na Tanzania Prisons, Salum Kihimbwa ni mchezaji huru.

Erick Kyaruzi Mopa Geita Gold

Erick Kyaruzi Mopa Geita Gold

Beki wa Geita Gold, Erick Kyaruzi maarufu Mopa amemaliza mkataba wake ndani ya timu hiyo hivyo yupo huru.

Haruna Kassim Shabani Tiote Mtibwa Sugar

Haruna Kassim Shabani Tiote Mtibwa Sugar

Mkataba wa Haruna Kassim Shabani maarufu Tiote na Mtibwa Sugar umemalizika na Sasa ni mchezaji huru.

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , , , ,

Comments are closed.