NAFASI za Kazi Wilaya ya Mwanga 08-03-2024
NAFASI za Kazi Wilaya ya Mwanga 08-03-2024
NAFASI za Kazi Wilaya ya Mwanga 08-03-2024,Nafasi za kazi wilaya ya mwanga 08.03.2024 pdf, Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Leo March 08-2024, Ajira Mpya Wilaya ya Mwanga Leo March 2024.
POST DEREVA DARAJA II – 2 POST
EMPLOYER Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
APPLICATION TIMELINE: 2024-03-08 2024-03-22
JOB SUMMARY NIL
DUTIES AND RESPONSIBILITIES
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari; - Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
- Kufanya usafi wa gari; na
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE
- Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
- Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
REMUNERATION TGS B
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini;
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili; - Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Cheti cha Kompyuta, Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards) “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa Recruitment Portal’).
- Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Tangazo Limetolewa na;
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA MWANGA
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 22 Machi, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
MKURUGENZI MTENDAJI (W),
HALMASHAURI YA WILAYA YA MWANGA,
S.L.P.716
MWANGA
CLICK HERE TO APPLY
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MWANGA 08-03-2024 DOWNLOAD PDF
CHIMBUKO/ASILI YA WILAYA YA MWANGA
- Kihistoria tangu nyakati za Ukoloni, eneo la miinuko ya Kusini mwa Mlima Kilimanjaro na kati ya miinuko ya Usambara –Tanga pamoja na tambarare zake, na mgawanyo wa kiutawala uliitambua jina UPARE kama neno la kutamkwa kama Wilaya ya Pare. Eneo hili lilikuwa na utawala wake wa wenyeji ambao tena ulitajwa kama Pare ya Kaskazini na Pare ya Kusini. Ambapo mwaka 1926 Chifu Kibacha Singo aliitisha machifu wote kwa lengo la kuunganisha wapare wote, hivyo mwaka 1928 wilaya ya Pare ilizaliwa
- WILAYA YA PARE NA VIONGOZI WAKE
Wilaya ya Pare ilikuwa inaongozwa na Machifu tisa (9) ambao kwa umoja wao walikuwa wanabadilishana uongozi kila baada ya mwaka mmoja.
Machifu hao ni kama ifuatavyo.
- SABUNI NAGUVU – USANGI
- MINJA KUKOME – UGWENO
- KIBACHA SINGO – SAME
- MBWANA YATERI (KIGHONO) – GONJA
- DAUDI SEKIMANGA MANENTO – MAMBA
- YUSUFU MAPOMBE – MBAGA
- CHAUKA SAIDI SADI – HEDARU
- RUBENI SHAZIA – SUJI
- IFOLONG’O MAKANGE – CHOME/MAKANYA
Machifu hawa walifanya kazi kwa kuzingatia matakwa ya wakoloni. Ili kuimarisha ulinzi katika eneo la hawa machifu palikuwa na walinzi waliokuwa wakiitwa Wachili, pamoja na kazi zao walihakikisha kuwa Chifu anakuwa katika hali ya usalama hivyo walipewa maeneo ya kuishi jirani na machifu. Kazi mojawapo ya Machifu ilikuwa ni kukusanya kodi ( Poly Tax ). Hata hivyo mnamo miaka ya hamsini machifu walishindwa kukidhi haja ya wakoloni hivyo chini yao wakaanzishwa Walao ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kukusanya kodi. Kwa kipindi hiki badala ya walao ni Makatibu Tarafa. Enzi za machifu palikuwa na Area Commissioner (AC) ambao kwa namna nyingine waliitwa Bwana shauri kwani hao ndio walikuwa ni Mahakimu katika ngazi ya wilaya.
MAKABILA/LUGHA.
Wilaya ya Pare tangu zamani ilikuwa na wakazi wenye lugha mbili ( 2), kwa Pare zote za Kusini na Kaskazini lugha kuu ni Kipare. Kwa Pare ya Kaskazini na hususani maeneo ya Ugweno iko lugha kuu ya Kigweno, yenye lafudhi inayoendana zaidi na Kichagga kuliko Kipare.
WILAYA YA MWANGA. (1979 – MPAKA SASA).
Wilaya ya Mwanga ilianzishwa tarehe 1, Julai,1979 baada ya Uhuru wa Tanganyika, kwa hivi sasa ni miongoni mwa wilaya Sita (6) za Mkoa wa Kilimanjaro, wilaya nyingine ni pamoja na Same, Rombo, Hai, Moshi na Siha. Wakati wa kuanzishwa ilikuwa miongoni mwa wilaya nne (4) ambazo zilikuwa Same, Moshi na Rombo, kabla ya kuanzishwa kwa wilaya mpya za Hai na Siha.
UTAWALA
Wakati wa kuanzishwa Wilaya ya Mwanga ilikuwa na Tarafa 4 za Mwanga, Ugweno, Usangi na Lembeni kabla ya kuanzishwa Tarafa mpya ya Jipe Ndea. Wilaya ilikuwa na Kata 16, Vijiji 53, na Jimbo moja la uchaguzi. Kwa sasa Wilaya ina Tarafa 5 za Jipe Ndea, Mwanga, Lembeni, Usangi na Ugweno na ina Mamlaka ya Mji Mdogo 1 yenye Vitongoji 12. Wilaya ina Kata 19 za Mgagao, Lembeni, Kileo, Lang’ata, Kirya, Kivisini, Kwakoa, Toloha, Mwaniko, Kifula, Msangeni, Shighatini, Kighare, Chomvu, Ngujini, Kilomeni, Kigonigoni, Kirongwe na Jipe, kuna vijiji 72 na Vitongoji 272.
UKUBWA WA ENEO
Ukubwa wa eneo la Wilaya ni kilomita za mraba 2641 kati ya hizo eneo la ardhi ya nchi kavu ni kilometa za mraba 2,558.6 na eneo la maji ni kilometa za mraba 82.4 ambapo Km 52 za mraba ni eneo la maji ya bwawa la Nyumba ya Mungu na Km 26.4 za mraba ni eneo la maji ya Ziwa Jipe.
WATU NA MAKAZI
Wakati inaanzishwa Wilaya ya Mwanga mwaka 1979 ilikuwa na wakazi wapatao 74,620 na kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya 2022 Wilaya ilikuwa na idadi ya watu 148, 763, ambapo wanaume walikuwa 72,157, na wanawake walikuwa ni 76,606, na jumla ya kaya zilikuwa ni 38,847.
HALI YA HEWA.
Wilaya inapata mvua kati ya millimita 400- 600 kwa maeneo ya Nyanda za Chini na kati ya millimita 800-1,200 kwa maeneo ya Nyanda ya Juu. Kuna misimu miwili ya mvua Vuli na Masika. Vuli huanza mwezi Oktoba hadi Desemba na Masika huanza mwezi Machi hadi Juni. Maeneo ya Nyanda ya Juu hupata mvua zote za Vuli na Masika. Wilaya hupata upepo mkali unao vuma tokea upande wa Mashariki kuelekea Magharibi, kiwango cha joto ni kati ya Nyuzi 14 sentigredi hadi Nyuzi 32 sentigredi hasa kwa mwezi Januari.
SHUGHULI ZA KIUCHUMI
1. KILIMO.
- Wilaya ya Mwanga ni mojawapo ya wilaya ambazo zinapata mvua haba kila mwaka hivyo mazao yanayolimwa kwa kutegemea mvua hayana uhakika. Kwa wakazi wanaoishi milimani wanategemea kilimo cha ndizi, maharage kama mazao ya chakula na kahawa kama zao la biashara. Kwa miaka ya tisini uzalishaji wa zao la kahawa ulipungua sana kutokana na pembejeo kuwa ghali mno. Wakulima wa kahawa walianzisha chama cha ushirika VUASU ili kuimarisha soko la biashara. Zao la kahawa ndilo liliwasaidia sehemu ya wakazi wa Mwanga kusomesha watoto.
Kwa upande wa tambarare ya Mashariki na Magharibi kuna kilimo cha umwagiliji ambapo zao maarufu ni mahindi na mpunga kwa ajili ya biashara.
Asilimia 85 ya wananchi wanaishi vijijini. Uchumi wa wilaya unategemea sana kilimo, ufugaji, uvuvi na sehemu ndogo wanajishughulisha na biashara ndogo ndogo. Mazao makubwa ya biashara yanayolimwa ni Kahawa,na Mkonge . Mazao ya chakula ni Mahindi, Maharage, Ndizi, Mihogo, Viazi vitamu na Mpunga.
2. UFUGAJI.
Ufugaji unakwenda sambamba na kilimo kwani unachangia Wananchi kuinua kipato chao. Kwa takwimu za mwaka 2016/17 Wilaya ina idadi ya Ng’ombe 117,007 wa kisasa wakiwa 14, 398 na kienyeji wakiwa 102, 609, Mbuzi 151,109, Kondoo 67, 102, Nguruwe 616, Sungura 196, Kuku 252 200, na Bata 2, 340, Punda 1, 317, Ngamia 8. Mifugo hii huuzwa kwa ajili ya kujipatia kipato. Pia Ng’ombe hutoa maziwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kuuza ili kupata fedha za kujikimu kimaisha, na ngozi huuzwa katika masoko ya ngozi ndani na nje ya Wilaya na kuongeza mapato ya Wafugaji.
3. UVUVI.
Kuna shughuli za Uvuvi katika Bwawa la Nyumba ya Mungu ambao ulianza mwaka 1969 baada ya Bwawa kujengwa. Pia kuna shughuli za uvuvi katika Ziwa Jipe ambapo wavuvi pamoja na wananchi katika maeneo hayo hujipatia mapato kutokana na uvuvi na biashara ya uvuvi. Samaki wanaovuliwa huuzwa ndani na nje ya Wilaya ya Mwanga.
BIASHARA.
Wilaya ina idadi ya biashara zifuatazo:- Baa na ‘’Grocery’’160, Maduka ya rejareja na Vioski 520, Maduka ya jumla 3, Mikahawa 80, Gereji 5 ,Hotel 1, Motel 6, Nyumba za kulala wageni 18, na kuna Vituo vya Mafuta 4 vinavyofanya kazi, na maduka ya hardware 14.
5. UFINYANZI.
- Pamoja na kilimo wakazi wa wilaya ya Mwanga tangu hapo awali walijikita katika biashara ya kutengeneza vyungu hasa akina mama wa Usangi na kuviuza Moshi na Arusha hata Mombasa.
UONGOZI WA WILAYA YA MWANGA BAADA YA UHURU
Baada ya kuondolewa kwa utawala wa Machifu mwaka 1963, uongozi wa kiwilaya uliwekwa chini ya Wakuu wa Wilaya. Wakuu wa Wilaya (Area Commissioner) katika Wilaya ya Pare toka mwaka 1962 hadi 1979 walikuwa wafuatao:-
Na. |
Jina la Wakuu wa Wilaya |
Muda |
1 |
BWANA AMSIRONG ( MZUNGU) |
1962 |
2 |
KAUGAHUA |
1962 – 1963 |
3 |
MBWANA KIHERE |
1963 – 1965 |
4 |
J. GWAHU |
1965 – 1967 |
5 |
MADENGE |
1967 – 1969 |
6 |
RWECHUNGURA |
1969 – 1972 |
7 | NYEMELE |
1972 – 1975 |
8 | MWAKATOBE |
1975 – 1979 |
ORODHA YA WAKUU WA WILAYA TOKA WILAYA YA MWANGA ILIPOANZISHWA MWAKA 1979
NA. |
JINA KAMILI |
MWAKA ALIOANZA |
MWAKA ALIO ONDOKA |
1 | Bi Salome Philemoni Nyiti |
1979 |
1980 |
2 | Bw. Adolfu Abeli Mwakyusa |
1980 |
1981 |
3 | Bw. Pius Mkongoti |
1981 |
1986 |
4 | Bw. B. K. Sanga |
1986 |
1992 |
5 | Capt. T. L.A. Mwabeza |
1992 |
1997 |
6 | Bw. John Tuppa |
1997 |
2001 |
7 | Bw. Rubeni Ole – Kuney |
2001 |
2005 |
8 | Bw. Jordan O. Rugimbana |
2005 |
2009 |
9 | Bw. Athumani Hassani Mdoe |
2009 |
2011 |
10 | Shaibu I. Ndemanga |
2012 |
2016 |
11 | Aaron Y. Mbogho |
2016 |
2019 |
12 | Thomas Cornel Apson |
2019 |
2021 |
13 | Abdallah Mussa Mwaipaya |
2021 |
Mpaka sasa |
Ramani ya wilaya ya mwanga, Halmashauri ya wilaya ya mwanga, Shule za msingi wilaya ya mwanga, Mwanga District Profile, Historia ya wilaya ya mwanga,Vijiji vya wilaya ya mwanga, Mwanga district council address.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania March 06-2024
- USAJILI wa Watahiniwa wa Kujitegemea CSEE NA FTNA 2024
- RITA Uhakiki wa Vyeti vya Kuzaliwa na Vifo
- JINSI ya Kuangalia Majibu ya Uhakiki RITA
- RITA Utaratibu na Muongozo wa Kuhakiki Vyeti HESLB
- RITA Uhakiki wa Online System 2023/2024
- FAHAMU Kitambulisho Chako Cha NIDA Kilipo
- JINSI ya Kupata Police Loss Report Online
- AINA za Madaraja ya Leseni za Udereva
- JINSI ya Kupata Leseni ya Biashara Online
- JINSI ya Kupata TIN Number Online
- JINSI ya Kulipia Vifurushi vya Azam TV
- OUT yakaribisha maombi ya Udahili Muhula wa Kwanza 2023/2024
- MO Dewji Tajiri namba 12 Barani Africa 2024
- FOMU ya Maombi ya Kujiunga na VETA Tanzania 2024
- ORODHA ya Vyuo vya Ualimu Tanzania
- MFUMO wa Maombi ya Ajira Za Walimu OTEAS 2024/2025
- MSIMAMO NBC Championship 2023/2024
- Haya hapa Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- SHULE 10 Bora Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- MATOKEO Ya Darasa la Nne 2023/2024
- MATOKEO ya Kidato Cha Pili 2023/2024
- JINSI ya Kuangalia Matokeo Kidato Cha Nne 2023/2024
- ADA za Lipa kwa Airtel Mitandao Yote
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024
- TETESI Za Usajili Yanga SC Dirisha Dogo 2023/2024
- Ada/makato ya Lipa kwa M-pesa, Lipa kwa Simu
- ORODHA ya Vilabu Bora Afrika November 2023 (IFFHS Club Ranking)
- MSIMAMO Kundi D CAF Champions League 2023/2024
- MSIMAMO Wa Kundi B CAF Champions League Standings 2023/2024
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- MSIMAMO NBC Premier League 2023/2024
- WAFUNGAJI Wanaoongoza Magoli NBC Premier League 2023/2024
- KIKOSI cha Yanga SC msimu wa 2023/2024
- RATIBA Kamili Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Simba SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Yanga SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya England (EPL 2023/2024)
- KIKOSI cha Simba SC msimu wa 2023/2024
Tags: Ajira Mpya Wilaya ya Mwanga Leo March 2024., Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Leo March 08-2024, NAFASI za Kazi Wilaya ya Mwanga 08-03-2024, Nafasi za kazi wilaya ya mwanga 08.03.2024 pdf