NAFASI za Kazi Wilaya ya Mpwapwa 11-03-2024
NAFASI za Kazi Wilaya ya Mpwapwa 11-03-2024
NAFASI za Kazi Wilaya ya Mpwapwa 11-03-2024,Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa 11-03-2024, Www Dodoma City Council go tz, Mpwapwa Tanzania, Mpwapwa villages, Vijiji vya mpwapwa,Www Mpwapwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa anawatangazia
Wananchi wote Raia wa Tanzania wenye sifa zinazohitajika kuomba kujaza nafasi wazi baada ya kupokea kibali cha ajira mbadala chenye Kumb Na. FA.228/613/01/A/073 cha tarehe 12 Februari,2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III (NAFASI 1)
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne na kuendelea.
- Awe amefuzu mafunzo ya Astashahada/Cheti NTA/LEVEL 5 katika moja ya fani
zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii au Sayansi ya Jamii kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali . - HESLB Dirisha la Kuomba Mkopo March Lafunguliwa
KAZI NA MAJUKUMU
- Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao kuwa mlinzi wa Amani na msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji
- Kuratibu na kusimamia upangaji na utelekezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Kijiji
- Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
- Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha Wananchi katika kuandaa na kutekeleza mkakati wa kuondoa njaa umaskini na
kuongeza uzalishaji mali - Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji
- Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika Kijiji
- Kupokea kusikiliza na kutatua malalamiko ya migogoro ya Wananchi
- Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji na
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata
NAFASI za Kazi Wilaya ya Mpwapwa 11-03-2024
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya mshahara ya Serikali ngazi ya Mshahara itakuwa TGS B
MAELEZO/ MASHARTI YA JUMLA
- Mwombaji awe Raia wa Tanzania ambaye ana umri si zaidi ya miaka 45 na sio pungufu ya Miaka 18.
- Waombaji wenye ulemavu wnahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulemavu walionao kwa
ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. - Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) yenye Anwani inayotumika, namba ya simu na Anuani ya barua pepe (Email address) pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Matokeo ya muda (Provisional/Testimonials/Statement of results) havitakubaliwa.
- Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Wombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokua kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe iapasavyo.
viii) Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na Wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyokatika waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010. - Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mafunzo mbali
mbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. - Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (NACTE na NACTE)
- Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahausika watachukuliwa hatua za kisheria
- Barua ya maombi itatakiwa iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni Jumanne, tarehe 21 Machi, 2024.
CLICK HERE TO APPLY
MUHIMU: kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa,
S.L.P 12,
MPWAPWA.
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa Ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https:portal.ajira.go.tz/ (anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MPWAPWA 11-03-2024 DOWNLOAD PDF DOCUMENT HERE
Historia
Jiografia ya wilaya ya Mpwapwa
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ni miongoni mwa Halmashauri nane (8) za Mkoa wa Dodoma. Makao makuu yapo umbali wa km.120 kutoka makao makuu ya Mkoa wa Dodoma.
Halmashauri ipo kati ya latitude 6°00” na 7°00” Kusini mwa mstari wa Ikweta na Longitudo 35°45” na 35°00” Mashariki mwa mstari wa ‘Greenwich’.
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa inapakana na Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kwa upande wa kaskazini, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa upande wa magharibi. Upande wa mashariki inapakana na Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa (mkoa wa Morogoro) na kusini inapakana na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa (Mkoa wa Iringa).
Ukubwa wa eneo
Wilaya ina eneo la kilometa za mraba 7,479 sawa na (18.35%) ya eneo lote la Mkoa wa Dodoma. Eneo hili ambalo ni sawa na hekta 737,900 linatumika kwa shuguli za kilimo, ufugaji, hifadhi ya misitu na makazi
Muundo wa Halmashauri ya Wilaya Kiutawala
Halmashauri ya Wilaya ina Majimbo 2 ya Uchaguzi, Tarafa 4, Kata 33, Vijiji 113, Vitongoji 575 na Mitaa 18.
Idadi ya Watu
Kutokana na Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Halmashauri ya Wilaya ilikadiriwa kuwa na wakazi 305,056 ambapo Wanaume wakiwa 147,306 (48.3%), Wanawake 157,750 (51.7%) na Kaya 66,316. Aidha, kwa mwaka 2016 kwa kutumia ukuaji wa asilimia 2.1, inakadiriwa kuwa na wakazi wapatao 331,500 kati yao Wanaume 162,435, na Wanawake 169,065 wanaoishi katika Kaya 72,065. Mgawanyo wa idadi ya watu kitarafa kwa ulinganisho wa Idadi ya Watu Matokeo ya Sensa ya Mwaka 2012 na makadirio ya watu mwaka 2016
Dira na Dhima
Dira
Kuwa Taasisi yenye kujali Wateja katika utoaji wa huduma Bora kwa Maendeleo Endelevu ifikapo 2025.
Dhima
Kutoa huduma Bora za kijamii na Kiuchumi kwa wateja wetu, kwa kuzingatia misingi ya Utawala Bora.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania March 06-2024
- USAJILI wa Watahiniwa wa Kujitegemea CSEE NA FTNA 2024
- RITA Uhakiki wa Vyeti vya Kuzaliwa na Vifo
- JINSI ya Kuangalia Majibu ya Uhakiki RITA
- RITA Utaratibu na Muongozo wa Kuhakiki Vyeti HESLB
- RITA Uhakiki wa Online System 2023/2024
- FAHAMU Kitambulisho Chako Cha NIDA Kilipo
- JINSI ya Kupata Police Loss Report Online
- AINA za Madaraja ya Leseni za Udereva
- JINSI ya Kupata Leseni ya Biashara Online
- JINSI ya Kupata TIN Number Online
- JINSI ya Kulipia Vifurushi vya Azam TV
- OUT yakaribisha maombi ya Udahili Muhula wa Kwanza 2023/2024
- MO Dewji Tajiri namba 12 Barani Africa 2024
- FOMU ya Maombi ya Kujiunga na VETA Tanzania 2024
- ORODHA ya Vyuo vya Ualimu Tanzania
- MFUMO wa Maombi ya Ajira Za Walimu OTEAS 2024/2025
- MSIMAMO NBC Championship 2023/2024
- Haya hapa Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- SHULE 10 Bora Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- MATOKEO Ya Darasa la Nne 2023/2024
- MATOKEO ya Kidato Cha Pili 2023/2024
- JINSI ya Kuangalia Matokeo Kidato Cha Nne 2023/2024
- ADA za Lipa kwa Airtel Mitandao Yote
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024
- TETESI Za Usajili Yanga SC Dirisha Dogo 2023/2024
- Ada/makato ya Lipa kwa M-pesa, Lipa kwa Simu
- ORODHA ya Vilabu Bora Afrika November 2023 (IFFHS Club Ranking)
- MSIMAMO Kundi D CAF Champions League 2023/2024
- MSIMAMO Wa Kundi B CAF Champions League Standings 2023/2024
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- MSIMAMO NBC Premier League 2023/2024
- WAFUNGAJI Wanaoongoza Magoli NBC Premier League 2023/2024
- KIKOSI cha Yanga SC msimu wa 2023/2024
- RATIBA Kamili Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Simba SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Yanga SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya England (EPL 2023/2024)
- KIKOSI cha Simba SC msimu wa 2023/2024
Tags: Mpwapwa Tanzania, Mpwapwa villages, NAFASI za Kazi Wilaya ya Mpwapwa 11-03-2024, Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa 11-03-2024, Vijiji vya mpwapwa, Www Dodoma City Council go tz, Www Mpwapwa.