RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Ngara June 04-2024

Filed in Ajira by on 04/06/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Ngara June 04-2024

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Ngara June 04-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Leo June 04-2024, Nafasi za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Leo June 2024.

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Ngara June 04-2024

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Ngara June 04-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Leo June 04-2024, Nafasi za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Leo June 2024.

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA NGARA 06-06-2024

Kufutia kutolewa kwa kibali cha Ajira Mbadala chenye Kumb.Na.FA.228/613/01/B/005 cha
terehe 22/04/2024 na Kumb.Na. FA.228/613/01/C/016 vya tarehe 25 Machi,2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara anawatangazia Watanzania
wote wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 02 za Mtendaji wa Kijiji III kama
inavyoonekana hapa chini:-

MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – (NAFASI 02)

SIFA ZA MWOMBAJI.

  • Awe na elimu ya kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).
  • Awe na cheti cha Astashahada (Technician Certificate- NTA LEVEL 5) katika moja ya fani zifuatazo: – Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

MAJUKUMU YA KAZI.

  • Afisa masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.Kusimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na Mali zao, Kuwa mlinzi wa Amani na
  • Msimamizi wa Utawala bora katika kijiji.
  • Kuratibu na Kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji.
  • Katibu wa Mikutano yote ya Halmashauri ya kijiji.
  • Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheriana Taratibu.
  • Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika Eneo lake na kuhamasisha katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali.
  • Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika kijiji.
  • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji.

SELECTION za Form Five na Vyuo vya Kati 2024

  • Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji.
  • Kupokea, Kusikiliza na Kutatua Malalamiko na Migogora ya Wananchi.
  • Kusimamia Utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji.
  • Atawajibika kwa mtendaji wa kata.

MSHAHARA.
Kwa kuzingatia Ngazi ya Mishahara ya Serikali yaani TGS B

MASHARTI KWA UJUMLA.

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya
    taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma;
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae)
    yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika;
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa za kuingilia katika
    kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, – Chetivcha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards);
  • “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa nabvimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 18 June, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vya Elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-

Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 30,
NGARA.

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye Mfumo wa Kieletroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana
kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal“).

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

DONWLOAD PDF DOCUMENT HAPA

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , ,

Comments are closed.