TAHSUSI mpya 49 zaongezwa Kidato cha Tano 2024
TAHSUSI mpya 49 zaongezwa Kidato cha Tano 2024
TAHSUSI mpya 49 zaongezwa Kidato cha Tano 2024, Combinations mpya 49 za Kidato cha Tano 2024, Serikali yatangaza Tahsusi mpya za Kidato cha Tano 2024, Serikali yatangaza Tahsusi mpya 49 za Kidato Cha Tano 2024,New 65 Form five Combinations 2024,orodha ya tahasusi za kidato cha Tano zitakazotumika kuanzia mwezi July 2024.
Ofisi ya Rais- TAMISEMI imetoa fursa kwa wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2023 kuongeza au kufanya marekebisho ya machaguo mapya ya tahasusi kwa kuongeza tahasusi kutoka 16 hadi 49 na kufikia jumla ya tahasusi 65.
TAHSUSI mpya 49 zaongezwa Kidato cha Tano 2024
Ofisi ya Rais- TAMISEMI Leo March 20 imetoa taarifa muhimu kwa wahitimu wa Kidato cha Nne mwaka 2023 kuhusu fursa ya kubadilisha machaguo ya Tahasusi za Kidato cha Tano na Kozi za Vyuo vya Ualimu, Vyuo vya Kati na Elimu ya Ufundi kwenye mfumo wa
kielektroniki wa uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na Kidato cha Tano na Vyuo.
Ikiwa ni maandalizi ya awali ya uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga Kidato cha Tano na Vyuo vya Serikali
Mwaka 2024.
Itakumbukwa kuwa Serikali imekuwa ikitoa fursa kwa wahitimu wa
Kidato cha Nne kufanya mabadiliko ya machaguo ya Tahasusi (combination) na Kozi mbalimbali walizozichagua kupitia Fomu ya
Uchaguzi (Selform.) Fursa hii huwawezesha wanafunzi kurekebisha machaguo yao kulingana na ufaulu waliopata kwenye matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).
Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI imekamilisha zoezi la awali la kuingiza kwenye kanzidata taarifa zilizo kwenye Fomu za Uchaguzi za wanafunzi kama zilivyojazwa na wanafunzi wakiwa
shuleni.
Aidha, napenda mtambue kuwa Mabadiliko ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023 na Mitaala ya Elimu kwa Kidato cha Tano yameanza kutekelezwa, ambapo
utekelezaji huo umehusisha uanzishaji wa Tahasusi mpya 49, kutoka 16 zilizokuwepo awali hadi kufikia tahasusi 65.
Hizi Hapa Combination Mpya Kidato cha Tano
Tahasusi hizo mpya zitakazoanza kutekelezwa Julai, 2024 zipo katika makundi saba (7) ambayo ni:
- Tahasusi za Sayansi ya Jamii;
- Tahasusi za Lugha;
- Tahasusi za Masomo ya Biashara; Tahasusi za Sayansi;
- Tahasusi za Michezo;
- Tahasusi za Sanaa; na
- Tahasusi za
Elimu ya Dini.
Orodha ya masomo na Tahasusi zitakazoanza kutekelezwa Julai, 2024 (Rejeeni kiambatisho Na.1)
Kukamilika kwa zoezi hili kunatoa fursa kwa wanafunzi kuweza kufanya mabadiliko ya machaguo/ tahasusi/ kozi kwa njia ya mtandao (online).
Baada ya wanafunzi kufanya marekebisho yao, kanzidata hiyo ndiyo itakayotumika kuwachagua na kuwapangia nafasi za Kidato cha Tano na Kozi mbalimbali katika Vyuo vya Kati
na vya Elimu ya Ufundi kwa kuzingatia sifa za ufaulu na machaguo yao.
Ofisi ya Rais – TAMISEMI inatoa fursa kwa wahitimu wa Elimu ya
Sekondari Kidato cha Nne mwaka 2023 kubadili machaguo yao ili kutoa nafasi zaidi kwa Mwanafunzi kusoma tahasusi au kozi itakayomwandaa kuwa na utaalam stahiki katika maisha yake ya
baadaye.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba wakati wa ujazaji wa fomu za machaguo ya awali, tahasusi mpya 49 hazikuwepo kwenye orodha ya machaguo na pia matokeo ya mtihani wa kuhitimu Kidato
cha Nne hayakuwa yametoka kumuwezesha mwanafunzi kuweza
kuwa na machaguo mazuri zaidi kulingana na ufaulu wake.
Hivyo, zoezi hili litatoa fursa zaidi ya wanafunzi kuongeza machaguo na
kufanya machaguo mapya ya Tahasusi na Kozi.
Napenda kuwasihi wazazi/walezi kushiriki katika zoezi hili kwa kushauriana na watoto wao katika kufanya machaguo sahihi kulingana na ufaulu wao.
Combination mpya kidato cha tano, Tahasusi mpya 2024 pdf download,
Selform Tamisemi go tz 2024, Combination za Form five PDF, Tahasusi Mpya pdf, Jinsi ya Kubadilisha Combination Online,Tahasusi mpya tamisemi pdf, Selection Form Five 2024.
Kwa umuhimu huo, wahitimu wote wanahimizwa kufanya marekebisho ya machaguo ya tahasusi na kozi kulingana na ufaulu wao, kwa kuingia kwenye Mfumo wa Uchaguzi wa Wanafunzi
(Student Selection MIS) unaopatikana kupitia kiunganishi cha selform.tamisemi.go.tz.
Aidha, maelekezo kwa wahitimu na jinsi
ya kufanya mabadiliko yanapatikana kwenye mfumo wa uchaguzi
wa wanafunzi.
Ili kuingia kwenye mfumo itabidi mhitimu atumie Namba ya Mtihani wa kuhitimu Kidato cha Nne mwaka 2023,
Jina lake la Mwisho, Mwaka wa Kuzaliwa na Alama ya Ufaulu aliyopata kwenye somo atakaloulizwa na mfumo au swali lolote atakaloulizwa.
Ni matumaini yangu kuwa wahitimu wote watatumia kwa ukamilifu fursa waliyopewa ya kubadilisha Tahasusi na Kozi kulingana na ufaulu waliopata na kutumia fursa ya kuchagua tahasusi mpya zitakazoanza kufundishwa Julai, 2024.
Pia wataweza kusoma tahasusi/kozi ambazo wamefaulu vizuri ama wana malengo nazo zaidi.
Zoezi la kubadilisha tahasusi na vyuo linaanza rasmi tarehe 20 Machi, 2024 hadi tarehe 30 Machi, 2024.
Wanafunzi, wazazi na walezi wanakumbushwa kushauriana kikamilifu ikiwa ni pamoja na
kupata ushauri wa kitaalam na kitaaluma kabla ya kufanya
mabadiliko ya tahasusi au Kozi.
Ninawasisitiza wanafunzi, wazazi/ walezi kutumia muda huo vyema
ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza mara baada ya
matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo kutangazwa.
Ni muhimu kuzingatia muda uliotolewa
wa kufanya marekebisho ili ratiba ya kuwachagua na kuwapangia
shule na vyuo iweze kuendelea kwa muda uliopangwa.
Baada ya matokeo ya kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo kutangazwa, Ofisi haitashughulikia changamoto hizo kwa kuwa fursa ya kufanya mabadiliko hayo imeshatolewa.
Huduma hii ya kubadilisha tahasusi ni bure na endapo wanafunzi watapata changamoto, wawasiliane na Dawati la
Huduma la Mteja kupitia barua pepe: [email protected]
au kuwasiliana moja kwa moja na Kituo cha Huduma kwa Wateja kwa simu +255 262 160 210 na +255 735 160 210.
Aidha, pamoja na maelekezo hayo, kwa mwanafunzi, mzazi/mlezi atakayekuwa na suala linalohitaji maelezo au ufafanuzi zaidi aende katika Ofisi za Elimu za Mikoa na Halmashauri.
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Mhe. Mohammed O. Mchengerwa, (MB)
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS
(TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA)
Hizi ni orodha ya tahasusi za kidato cha Tano zitakazotumika kuanzia mwezi Julai mwaka 2024
Tahasusi kidato cha tano, Combination Mpya kidato cha tano 2024, Combination za Form five pdf, PMC combination jobs, Tahasusi Mpya 2024, Combination Za Form five 2024, A level combinations Tanzania, PMC combination in Tanzania, Combination za advance TAMISEMI, Jinsi Ya Kubadilisha Tahasusi, Combination za Arts.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania March 06-2024
- USAJILI wa Watahiniwa wa Kujitegemea CSEE NA FTNA 2024
- RITA Uhakiki wa Vyeti vya Kuzaliwa na Vifo
- JINSI ya Kuangalia Majibu ya Uhakiki RITA
- RITA Utaratibu na Muongozo wa Kuhakiki Vyeti HESLB
- RITA Uhakiki wa Online System 2023/2024
- FAHAMU Kitambulisho Chako Cha NIDA Kilipo
- JINSI ya Kupata Police Loss Report Online
- AINA za Madaraja ya Leseni za Udereva
- JINSI ya Kupata Leseni ya Biashara Online
- JINSI ya Kupata TIN Number Online
- JINSI ya Kulipia Vifurushi vya Azam TV
- OUT yakaribisha maombi ya Udahili Muhula wa Kwanza 2023/2024
- MO Dewji Tajiri namba 12 Barani Africa 2024
- FOMU ya Maombi ya Kujiunga na VETA Tanzania 2024
- ORODHA ya Vyuo vya Ualimu Tanzania
- MFUMO wa Maombi ya Ajira Za Walimu OTEAS 2024/2025
- MSIMAMO NBC Championship 2023/2024
- Haya hapa Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- SHULE 10 Bora Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- MATOKEO Ya Darasa la Nne 2023/2024
- MATOKEO ya Kidato Cha Pili 2023/2024
- JINSI ya Kuangalia Matokeo Kidato Cha Nne 2023/2024
- ADA za Lipa kwa Airtel Mitandao Yote
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024
- TETESI Za Usajili Yanga SC Dirisha Dogo 2023/2024
- Ada/makato ya Lipa kwa M-pesa, Lipa kwa Simu
- ORODHA ya Vilabu Bora Afrika November 2023 (IFFHS Club Ranking)
- MSIMAMO Kundi D CAF Champions League 2023/2024
- MSIMAMO Wa Kundi B CAF Champions League Standings 2023/2024
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- MSIMAMO NBC Premier League 2023/2024
- WAFUNGAJI Wanaoongoza Magoli NBC Premier League 2023/2024
- KIKOSI cha Yanga SC msimu wa 2023/2024
- RATIBA Kamili Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Simba SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Yanga SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya England (EPL 2023/2024)
- KIKOSI cha Simba SC msimu wa 2023/2024
Tags: Combinations mpya 49 za Kidato cha Tano 2024, New 65 Form five Combinations 2024, orodha ya tahasusi za kidato cha Tano zitakazotumika kuanzia mwezi July 2024., Serikali yatangaza Tahsusi mpya 49 za Kidato Cha Tano 2024, Serikali yatangaza Tahsusi mpya za Kidato cha Tano 2024, TAHSUSI mpya 49 zaongezwa Kidato cha Tano 2024