RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


EID El Fitr ni Leo Jumatano April 10-2024

Filed in Habari, Makala, Michezo by on 10/04/2024

EID El Fitr ni Leo Jumatano April 10-2024

EID El Fitr ni Leo Jumatano April 10-2024,Eid al-Fitr 2024,2024 eid ul-adha date, 2024 Eid ul Fitr date, Eid al fitr 2024 saudi arabia live, Ramadan 2024,Bakwata eid 2024, Eid ul Fitr 2024 UK Saudi Arabia,when is eid al-adha, Has saudi announced eid 2024,Sikukuu ya idd ni lini 2024.

EID El Fitr ni Leo Jumatano April 10-2024

EID El Fitr ni Leo Jumatano April 10-2024, Kamati ya kufuatilia miandamo ya mwezi ya BARAZA KUU LA JUMUIYA ZA ANSAAR SUNNAH TANZANIA (BASUTA), imewatangazia Waislamu wanaofunga na kufungua saumu kwa kufuata mwandamo wa mwezi unaoonekana na kuthibiti Kishari’ah popote pale Duniani ya kwamba siku ya Jumatatu tarehe 08 Aprili 2024 ilikuwa mwezi 29 Ramadhan, 1445 Hijriyyah.

Taarifa ya BASUTA ya jioni hii imeeleza kuwa kamati hiyo haijapokea taarifa ya kuthibiti kuandama mwezi wa Shawwal si kutoka ndani ya Tanzania wala kutoka nchi nyingine yoyote ile duniani hivyo tunakamilisha Siku 30 Ramadhan leo (jana) Jumanne tarehe 9 Aprili, 2024.

“Kamati imepokea taarifa za kutokuandama mwezi kutoka mamlaka mbali mbali za kutangaza mwezi katika nchi za Saudia, Qatar, U.A.E, Misri, Baharain, Kuweit, Yemen, Lebanon, Palestina, Iraq, Syria” imesema taarifa hiyo

“Kwa taarifa hizi, siku ya Jumatano tarehe 10 Aprili 2024 itakuwa ndiyo mwezi Mosi Mfungo wa Mosi (Shawwal) 1445 Hijriyyah Sikukuu ya ldul Fitr”

Kamati imefikia maamuzi haya kutokana hadithi iliyopokewa na Imam Bukhari na Muslim (Allah awarehemu) kutoka kwa Swahaba Abu Hureira (Allah amridhie) akieleza kuwa Mtume wa Allah (Allah amshushie rehma na amani) anasema:

“Fungeni kwa kuonekanwa kwake (mwezi) na fungueni kwa kuonekanwa kwake (mwezi). Na iwapo mtagubikwa (msiuone mwezi), basi kamilisheni hesabu ya mwezi siku thelathini”.

“Kwa mnasaba huu, uongozi wote wa BASUTA unawatakia Waislamu wote kheri ya Siku Kuu ya ldul Fitr mwaka 1445 Hijriyyah pamoja na kuwahimiza kutimiza kutoa Zakatul Fitr kabla ya kuswali swala ya ldd na pia kusherehekea Sikukuu ndani ya mipaka ya Kishari’ah kwa kujiepusha na yale yote yenye kumuudhi Allah (Subhaahuu Wa Taala)”

“Taarifa hii imethibitishwa na masheikh wajumbe wa Kamati ya BASUTA ya kufuatilia Mwandamo wa mwezi na iwapo tutapokea taarifa tofauti na hizi tulizozipokea wakati huu kuhusu kuandama mwezi, Kamati haitasita kuwajulisheni.”

EID El Fitr ni Leo Jumatano April 10-2024

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Tags: , , , , , , , , , ,

Comments are closed.