NAFASI 5 za Watendaji wa Kijiji Wilaya ya Bunda April 2024
NAFASI 5 za Watendaji wa Kijiji Wilaya ya Bunda April 2024
NAFASI 5 za Watendaji wa Kijiji Wilaya ya Bunda April 2024, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kuomba nafasi za kazi zilizotajwa hapo chini, baada ya kupokea Vibali vya Ajira vyenye Kumb. Na. FA.228/613/01/A/041,
Kumb. Na. FA.228/613/01/A/042, Kumb. Na. FA.228/613/01/A/043 na Kumb. Na. FA.228/613/01/A/045 vya tarehe 05 Februari, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora.
MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – (NAFASI 5).
SIFA ZA MWOMBAJI.
- Awe amehitimu elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI)
- Awe amehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti cha Technician Certificate (NTA Level 5) katika moja ya fani zifuatazo:- Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka katika
Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo – Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali. - NAFASI 2 za Mtendaji wa Kijiji Wilaya ya Mbarali April 2024
MAJUKUMU YA KAZI.
- Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji;
- Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao,
- Kuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora wa Kijiji;
- Kuratibu na Kusimamia upangaji wa Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji;
- Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji;
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
- Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na
kuongeza uzalishaji mali; - Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji;
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji:
- Mwenyekiti wa Kikao cha Wataalam waliopo katika Kijiji;
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
- Kusimamia Utungaji wa Sheria Ndogo za Kijiji; na
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
MSHAHARA.
Kwa kuzingatia Ngazi ya Mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa Mwezi.
MASHARTI KWA UJUMLA.
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma;
- Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika;
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwavkuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards);
- “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE). Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba,
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA 04-04-2024 DONWLOAD PDF
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 17 Aprili, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vya Elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda,
S.L.P 126,
BUNDA.
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye Mfumo wa Kieletroniki wa Ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal“).
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
KUTUMA MAOMBI BONYEZA HAPA
POST: MTENDAJI WA KIJIJI III – 5 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Bunda More Details |
2024-04-17 Login to Apply |
ABOUT BUNDA DISTRICT COUNCIL:
Bunda District Council is one of the Local Government Authorities established in 1984 under District Authority as the provision of section 8 and 9 of 1982 with effect of the first day of January, 1984.
LOCATION OF BUNDA DISTRICT:
Bunda District is located on the Western part of Mara region. The District is one of the Nine Local Authorities constitute Mara region. To the North is bordered by Musoma District Council and Butiama District, to the South by Lake Victoria and Simiyu Region, to the East by the Serengeti District, and to the West by Lake Victoria. Bunda District Council is located at an elevation of 1,225 meters above sea level. It is located 2° 0’0’’ S and 33°49’60’’E in Degrees Minutes Seconds.
NAFASI 5 za Watendaji wa Kijiji Wilaya ya Bunda April 2024
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania April 03-2024
- USAJILI wa Watahiniwa wa Kujitegemea CSEE NA FTNA 2024
- RITA Uhakiki wa Vyeti vya Kuzaliwa na Vifo
- JINSI ya Kuangalia Majibu ya Uhakiki RITA
- RITA Utaratibu na Muongozo wa Kuhakiki Vyeti HESLB
- RITA Uhakiki wa Online System 2023/2024
- FAHAMU Kitambulisho Chako Cha NIDA Kilipo
- JINSI ya Kupata Police Loss Report Online
- AINA za Madaraja ya Leseni za Udereva
- JINSI ya Kupata Leseni ya Biashara Online
- JINSI ya Kupata TIN Number Online
- JINSI ya Kulipia Vifurushi vya Azam TV
- OUT yakaribisha maombi ya Udahili Muhula wa Kwanza 2023/2024
- MO Dewji Tajiri namba 12 Barani Africa 2024
- FOMU ya Maombi ya Kujiunga na VETA Tanzania 2024
- ORODHA ya Vyuo vya Ualimu Tanzania
- MFUMO wa Maombi ya Ajira Za Walimu OTEAS 2024/2025
- MSIMAMO NBC Championship 2023/2024
- Haya hapa Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- SHULE 10 Bora Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- MATOKEO Ya Darasa la Nne 2023/2024
- MATOKEO ya Kidato Cha Pili 2023/2024
- JINSI ya Kuangalia Matokeo Kidato Cha Nne 2023/2024
- ADA za Lipa kwa Airtel Mitandao Yote
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024
- TETESI Za Usajili Yanga SC Dirisha Dogo 2023/2024
- Ada/makato ya Lipa kwa M-pesa, Lipa kwa Simu
- ORODHA ya Vilabu Bora Afrika November 2023 (IFFHS Club Ranking)
- MSIMAMO Kundi D CAF Champions League 2023/2024
- MSIMAMO Wa Kundi B CAF Champions League Standings 2023/2024
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- MSIMAMO NBC Premier League 2023/2024
- WAFUNGAJI Wanaoongoza Magoli NBC Premier League 2023/2024
- KIKOSI cha Yanga SC msimu wa 2023/2024
- RATIBA Kamili Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Simba SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Yanga SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya England (EPL 2023/2024)
- KIKOSI cha Simba SC msimu wa 2023/2024
Tags: NAFASI 5 za Watendaji wa Kijiji Wilaya ya Bunda April 2024