TANZIA Edward Lowassa afariki Dunia
TANZIA Edward Lowassa afariki Dunia
TANZIA Edward Lowassa afariki Dunia, Historia ya edward Lowassa,Edward Lowassa age,Edward Lowassa amefariki,Edward Lowassa afariki.
Makamu wa Rais wa Tanzania, Philip Mpango ametangaza kifo cha Waziri wa zamani wa Tanzania, Edward Lowassa aliyefariki leo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dar es Salaam leo Februari 10-2024.
Akizungumza kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia televisheni ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amesema, Lowassa amefariki baada ya kuugua magonjwa ya kujikunja utumbo, matatizo ya mapafu na shinikizo la damu.
“Hayati Edward Lowassa ameugua kwa muda mrefu na amekuwa akipatiwa matibabu tangu Januari 14, 2022 JKCI na baadaye akapelekwa kwa matibabu zaidi nchini Afrika Kusini na kurejea tena JKCI,” amesema.
Kutokana na kifo hicho, Rais Samia ametoa pole kwa ndugu, jamaa na rafiki.
“Aidha, Rais Samia ametangaza siku tano za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia leo Februari 10, 2024, taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitaendelea kutolewa na Serikali,” amesema Dk Mpango.
Dk Mpango aliyekuwa ziarani Wilaya ya Longido mkoani Arusha, alikatisha kazi hiyo na kuondoka na msafara wake kuelekea wilayani Monduli, ambako alitangaza taarifa ya kifo hicho kupitia TBC.
TANZIA Edward Lowassa afariki Dunia
Mfahamu Edward Ngoyayi Lowassa
Edward Ngoyayi Lowassa (amezaliwa 26 Agosti 1953) alikuwa ni mwanasiasa nchini Tanzania.
Alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa kumi wa nchi hiyo tarehe 30 Desemba 2005 akajiuzulu tarehe 7 Februari 2008 kwa kashifa ya Richmond. Mwaka 2015 alikuwa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo.
Lowassa ni mwenyeji na alikuwa mbunge wa Monduli katika Mkoa wa Arusha.
Alisoma shahada ya kwanza katika tamthilia kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, halafu shahada ya pili katika sayansi ya maendeleo ya jamii Chuo Kikuu cha Hull nchini Uingereza.
Nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika
Lowassa ni mwanasiasa mkongwe mwenye uzoefu mbalimbali katika siasa za nchini Tanzania, kwa kuwa aliwahi kushika vyeo mbalimbali katika serikali kama vile:
- Waziri mdogo wa mazingira na mapambano dhidi ya umaskini katika ofisi ya Makamu wa Rais (1988-2000)
- Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (1989-1990)
- Waziri mdogo wa haki na mambo ya bunge katika ofisi ya Makamu wa Rais (1990-1993)
- Mbunge wa Monduli tangu 1990
- Katika Disemba 2005 alipitishwa na bunge kuwa waziri mkuu wa Tanzania
Mwaka 1995 Edward Lowassa aliamua kuingia katika mchakato wa kumpata mgombea urais kwa tiketi ya CCM. Wakati huo Lowassa aliombwa na Umoja wa Vijana kupitia kikao cha baraza kuu la Taifa achukue fomu akiwa miongoni mwa wana CCM wanne ambao vijana waliamini wataweza kulisaidia Taifa kupiga hatua za haraka kuelekea maendeleo endelevu, wengine waliokuwa wametajwa na Umoja wa vijana ni Salim Ahmed Salim, Laurance Gama na jaji mstaafu Mark Bomani.
Katika hatua ya kuchagua majina 3 kati ya majina 11 yaliyoomba nafasi hiyo, Lowassa akawa hakupendekezwa, lakini hakununa wala kususa bali aliamini kuwa mwanamapinduzi mwenzie Jakaya Mrisho Kikwete ataweza kutekeleza dhamira aliyokuwa nayo ya kuwaletea Watanzania maendeleo, hivyo alirudi kwa makundi mbalimbali wakiwemo vijana wa CCM ambao walihoji kwa nini ameenguliwa, na yeye kwa utii mkubwa kwa CCM aliwataka vijana na viongozi wengine waheshimu maamuzi ya chama na kumuunga mkono Kikwete. Ikumbukwe kuwa mwana-CCM mwingine aliyekuwa anakubalika kwa umma Lowassa aliondoka mapema CCM kwa sababu ndogo tu ya kubadilishiwa wizara na kuamua kwenda chama cha NCCR mageuzi ambako aligombea uraisi kwa chama hicho na kuleta upinzani mkubwa.
Yapo maneno ya baadhi ya wanasiasa kwamba kutoteuliwa kugombea kwa Lowassa kulitokana na kuonekana anamiliki fedha nyingi akiwa na muda mfupi kwenye utumishi wa umma, lakini pia inasemekana kuwa wale waliohoji kukatwa kwa jina lake kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya Taifa, majibu yalikuwa, CCM iliamua kupeleka majina matatu kwenye mkutano mkuu ili wachague moja katika uwakilishi huo wa majina: walipenda apatikane mtu mzima mmoja, mwenye umri wa kati mmoja na kijana mmoja, watu hao ni mzee David Msuya ambae ni mtu mzima, Benjamini Mkapa ambae umri wake ulikuwa wa kati na kijana ambae ni Jakaya Kikwete.
Lakini maneno hayo ya baadhi ya wanasiasa hayakuishia hapo: wakadai baada ya Rais Mkapa kuchaguliwa, hakumteua Lowassa kwa kuwa aliagizwa na Mwalimu Nyerere[onesha uthibitisho] asimteue mpaka achunguzwe kama uwezo kiasi wa fedha alionao unatokana na mapato halali, kama siyo halali asimteue. Mwaka 1997 Rais Mkapa akamteua Lowassa kuwa Waziri wa nchi, ofisi ya makamu wa Rais mazingira.
Tarehe 7 Februari 2008 Lowassa alijiuzulu baada ya kushtakiwa kuwa ameshiriki katika kashfa ya Richmond. Kamati ya bunge iliwahi kuchungulia mkataba baina ya kampuni ya TANESCO na kampuni ya Richmond Development Company LLC kutoka Houston, Texas. Kamati ya wabunge watano chini ya mwenyekiti Harrison Mwakyembe ikaona mkataba huu ilikuwa kidanganyifu. Richmond ilipewa kazi ya kutengeneza megawati 100 za umeme kila siku baada ya ukame wa mwaka 2006 uliopunguza uwezo wa TANESCO kutoa umeme nchini kutokana na mitambo yake ya umememaji. Lakini mitambo ya dharura ya Richmond ilichelewa kufika nchini pia haikufanya kazi jinsi ilivyotakiwa[1]. Hata hivyo serikali ikaendelea kulipa zaidi ya dolar za Marekani 100,000 kila siku.
Kamati ya bunge ikaona ya kwamba Lowassa alishawishi azimio kuhusu mkataba na Richmond kwa kupuuza masharti ya kisheria na kinyume cha ushauri wa TANESCO. Baada ya kujadiliwa kwa taarifa ya kamati kwenye bunge Lowassa akajiuzulu pamoja na Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagima waliowahi kuwa mawaziri wa nishati.[2] Hata hivyo Lowassa alikataa ya kwamba alikuwa na hatia yoyote.
Mwaka 2014 Lowassa alisimamishwa na kamati kuu ya CCM baada ya kushtakiwa ya kwamba aliwahi kuanzisha kampeni ya kuwa mgombea wa urais kabla ya kipindi kilichokubaliwa na chama hiki.
Mwezi Mei 2015 hatimaye aliweza kuanzisha kampeni yake rasmi lakini kamati kuu ya CCM ilimwondoa katika orodha ya majina yaliyopelekwa kwa uteuzi huu ndani ya chama.
Lowassa akaondoka katika CCM na tarehe 28 Julai 2015 alijunga rasmi na chama cha upinzani cha CHADEMA.
Siku chache baadaye aliteuliwa kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CHADEMA mnamo Oktoba 2015. Kadiri ya Tume ya Uchaguzi alishindwa kwa kupata asilimia 39.97 za kura zote na mgombea wa CCM John Pombe Magufuli aliyepata 58.46%.
Lowassa aliendelea kuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chadema. Mwaka 2016 alitangaza ya kwamba hawezi kurudi kamwe CCM.
Kwenye Januari 2018 aliwahi kuwa na mazungumzo marefu na rais Magufuli. Tarehe 1 Machi 2019 alirudi kwenye chama chake cha awali CCM
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania February 07-2024
- USAJILI wa Watahiniwa wa Kujitegemea CSEE NA FTNA 2024
- RITA Uhakiki wa Vyeti vya Kuzaliwa na Vifo
- JINSI ya Kuangalia Majibu ya Uhakiki RITA
- RITA Utaratibu na Muongozo wa Kuhakiki Vyeti HESLB
- RITA Uhakiki wa Online System 2023/2024
- FAHAMU Kitambulisho Chako Cha NIDA Kilipo
- JINSI ya Kupata Police Loss Report Online
- AINA za Madaraja ya Leseni za Udereva
- JINSI ya Kupata Leseni ya Biashara Online
- JINSI ya Kupata TIN Number Online
- JINSI ya Kulipia Vifurushi vya Azam TV
- OUT yakaribisha maombi ya Udahili Muhula wa Kwanza 2023/2024
- MO Dewji Tajiri namba 12 Barani Africa 2024
- FOMU ya Maombi ya Kujiunga na VETA Tanzania 2024
- ORODHA ya Vyuo vya Ualimu Tanzania
- MFUMO wa Maombi ya Ajira Za Walimu OTEAS 2024/2025
- MSIMAMO NBC Championship 2023/2024
- Haya hapa Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- SHULE 10 Bora Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- MATOKEO Ya Darasa la Nne 2023/2024
- MATOKEO ya Kidato Cha Pili 2023/2024
- JINSI ya Kuangalia Matokeo Kidato Cha Nne 2023/2024
- ADA za Lipa kwa Airtel Mitandao Yote
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024
- TETESI Za Usajili Yanga SC Dirisha Dogo 2023/2024
- Ada/makato ya Lipa kwa M-pesa, Lipa kwa Simu
- ORODHA ya Vilabu Bora Afrika November 2023 (IFFHS Club Ranking)
- MSIMAMO Kundi D CAF Champions League 2023/2024
- MSIMAMO Wa Kundi B CAF Champions League Standings 2023/2024
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- MSIMAMO NBC Premier League 2023/2024
- WAFUNGAJI Wanaoongoza Magoli NBC Premier League 2023/2024
- KIKOSI cha Yanga SC msimu wa 2023/2024
- RATIBA Kamili Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Simba SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Yanga SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya England (EPL 2023/2024)
- KIKOSI cha Simba SC msimu wa 2023/2024
Tags: Edward Lowassa afariki., Edward Lowassa age, Edward Lowassa amefariki, Historia ya edward Lowassa, TANZIA Edward Lowassa afariki Dunia, TANZIA Edward Lowassa amefariki Dunia