SIMBA na Azam zathibitisha Kushiriki Kombe la Muungano Zanzibar 2024
SIMBA na Azam zathibitisha Kushiriki Kombe la Muungano Zanzibar 2024
SIMBA na Azam zathibitisha Kushiriki Kombe la Muungano Zanzibar 2024, Klabu za Simba na Azam FC zimethibitisha kushiriki michuano ya Kombe la Muungano inayoenda sambamba na Miaka 60 ya Sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zitakazoadhimishwa Aprili 26, huku Yanga ikichomoa.
Simba na Azam zilizopo katika Ligi Kuu Bara ndizo timu pekee za Tanzania Bara zilizothibitisha kushiriki katika michuano hiyo itakayoshirikisha pia timu za visiwani Unguja na Pemba.
Simba iliyopo nafasi ya tatu na Azam ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara zimethibitisha kushiriki michuano hiyo itakayoanza Aprili 23.
Akizungumza na Gazeti la Mwanaspoti, Rais wa Shirikisho la Soka Zanzibar(ZFF), Suleiman Mahmoud amesema, walikuwa kimya kwa muda kusubiri taarifa ya Simba kama watakuwepo au la, huku ya Azam ikithibitisha mapema ushiriki wao.
Rais hiyo ZFF amesema kuwa Yanga walitoa taarifa mapema kuwa hawataweza kushiriki kutokana na ratiba iliyonayo msimu huu.
“Nia ya michuano hii ni kuinua uhusiano kati ya Bara na Zanzibar kwa upande wa soka, lakini kuimarisha timu zetu za huku na biashara kwa ujumla kwani timu kubwa zinapocheza huwa kuna watazamaji na watalii wengi wanaokuja Zanzibar, amesema Suleiman na kuongeza;
“Bila kusahau kuongeza tuzo na uimara wa wachezaji, kwani wanapocheza michezo tofauti na yenye ushindani wa aina hii basi ni mazoezi tosha ya kujiboresha zaidi.
“Ni fursa kwa vipaji vilivyoko Zanzibar, kupata nafasi ya kuonekana na watu wengi hivyo ni rahisi kwao kupata ajira na kujulikana.” amesema.
Ratiba ya michuano hiyo inatarajiwa kutolewa muda wowote kuanzia sasa.
Mbali na Simba na Azam timu nyingine shiriki kwa mujibu wa Suleiman ni mabingwa Zanzibar KMKM na KVZ.
Michuano hiyo itachezwa kwenye Uwanja mpya wa New Amaan Complex na fainali itachezwa Aprili 27 siku moja baada ya sherehe za maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano.
Tanganyika na Zanzibar ziliungana Aprili 26, 1964 na kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa kwa sasa na Rais Samia Suluhu Hassan.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania April 03-2024
- USAJILI wa Watahiniwa wa Kujitegemea CSEE NA FTNA 2024
- RITA Uhakiki wa Vyeti vya Kuzaliwa na Vifo
- JINSI ya Kuangalia Majibu ya Uhakiki RITA
- RITA Utaratibu na Muongozo wa Kuhakiki Vyeti HESLB
- RITA Uhakiki wa Online System 2023/2024
- FAHAMU Kitambulisho Chako Cha NIDA Kilipo
- JINSI ya Kupata Police Loss Report Online
- AINA za Madaraja ya Leseni za Udereva
- JINSI ya Kupata Leseni ya Biashara Online
- JINSI ya Kupata TIN Number Online
- JINSI ya Kulipia Vifurushi vya Azam TV
- OUT yakaribisha maombi ya Udahili Muhula wa Kwanza 2023/2024
- MO Dewji Tajiri namba 12 Barani Africa 2024
- FOMU ya Maombi ya Kujiunga na VETA Tanzania 2024
- ORODHA ya Vyuo vya Ualimu Tanzania
- MFUMO wa Maombi ya Ajira Za Walimu OTEAS 2024/2025
- MSIMAMO NBC Championship 2023/2024
- Haya hapa Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- SHULE 10 Bora Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- MATOKEO Ya Darasa la Nne 2023/2024
- MATOKEO ya Kidato Cha Pili 2023/2024
- JINSI ya Kuangalia Matokeo Kidato Cha Nne 2023/2024
- ADA za Lipa kwa Airtel Mitandao Yote
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024
- TETESI Za Usajili Yanga SC Dirisha Dogo 2023/2024
- Ada/makato ya Lipa kwa M-pesa, Lipa kwa Simu
- ORODHA ya Vilabu Bora Afrika November 2023 (IFFHS Club Ranking)
- MSIMAMO Kundi D CAF Champions League 2023/2024
- MSIMAMO Wa Kundi B CAF Champions League Standings 2023/2024
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- MSIMAMO NBC Premier League 2023/2024
- WAFUNGAJI Wanaoongoza Magoli NBC Premier League 2023/2024
- KIKOSI cha Yanga SC msimu wa 2023/2024
- RATIBA Kamili Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Simba SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Yanga SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya England (EPL 2023/2024)
- KIKOSI cha Simba SC msimu wa 2023/2024
Tags: SIMBA na Azam zathibitisha Kushiriki Kombe la Muungano Zanzibar 2024