RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


GSM akubali Kujenga Uwanja wa Yanga

Filed in Michezo by on 12/02/2024

GSM akubali Kujenga Uwanja wa Yanga

GSM akubali Kujenga Uwanja wa Yanga, GSM Kujenga Uwanja wa Young Africans, Ghalib Said Mohammed akubali Kujenga Uwanja wa Yanga, Uwanja wa Yanga kujengwa wapi?, Uwanja mpya wa Yanga, Yanga kujengewa Uwanja,GSM Aridhia Kushiriki Kufanikisha Ujenzi Wa Uwanja Wa Kisasa Wa Yanga,GSM Kuijengea Yanga Uwanja wa Kisasa Jangwani.

GSM akubali Kujenga Uwanja wa Yanga

GSM akubali Kujenga Uwanja wa Yanga, GSM Kujenga Uwanja wa Young Africans, Ghalib Said Mohammed akubali Kujenga Uwanja wa Yanga, Uwanja wa Yanga kujengwa wapi?, Uwanja mpya wa Yanga, Yanga kujengewa Uwanja,GSM Aridhia Kushiriki Kufanikisha Ujenzi Wa Uwanja Wa Kisasa Wa Yanga,GSM Kuijengea Yanga Uwanja wa Kisasa Jangwani.

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amewataarifu Wanachama na Mashabiki wa Klabu hiyo kuwa Mdhamini/Mfadhili wa timu hiyo Ghalib Said Mohammed (GSM) atashiriki katika ujenzi wa Uwanja wa Yanga.

Hersi amesema kuwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati ya uongozi wa Yanga na GSM, sasa ni rasmi GSM atashiriki katika kufanikisha ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Yanga SC.

Taarifa rasmi kutoka kwa Rais wa Yanga Injinia Hersi Said.

Leo, Februari 11, 2024 Klabu yetu kongwe na yenye mafaniko zaidi nchini Tanzania, Young Africans Sports Club imefikisha miaka 89 tangu kuanzishwa kwake.

Nichukue fursa hii kuwapongeza sana Viongozi walionitangulia, Wazee, Wanachama, mashabiki na wapenzi walioshiriki kwenye safari ndefu ya kuijenga Klabu yetu iliyoshiriki kwenye matukio mengi ya Ki- taifa ikiwemo kutafuta Uhuru wa Nchi yetu na kuijenga Tasnia ya michezo, hali inayofanya kwa sasa, Young Africans SC kuwa tunu na sio Tanzania bali Afrika kwa ujumla.

Aidha, nichukue fursa hii kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki na Wanafamilia wote wa Young Africans SC kwa kumpoteza aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu yetu, Mzee Imani Madega, aliye- fariki siku ya jana.

Wakati huo huo, naungana na Watanzania wote kwenye maombolezo ya msiba wa kitaifa wa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa.

Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. Amen.

Katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu wa uongozi wangu kama Rais wa Klabu hii kwa kushirikiana na Kamati yangu tendaji, tumeweza kuwa na maendeleo makubwa kwenye maeneo mbalimbali, ikiwemo kiutawala, kimichezo na kimiundombinu.

Leo, tukiwa kwenye sherehe za miaka 89 za kuzaliwa kwa Klabu yetu, nina Habari njema ya kuwaeleza Wanachama na Mashabiki wa Klabu yetu ya Young Africans Sports Club.

GSM akubali Kujenga Uwanja wa Yanga, GSM Kujenga Uwanja wa Young Africans, Ghalib Said Mohammed akubali Kujenga Uwanja wa Yanga, Uwanja wa Yanga kujengwa wapi?, Uwanja mpya wa Yanga, Yanga kujengewa Uwanja,GSM Aridhia Kushiriki Kufanikisha Ujenzi Wa Uwanja Wa Kisasa Wa Yanga,GSM Kuijengea Yanga Uwanja wa Kisasa Jangwani.Baada ya mazungumzo ya muda mrefu na mdhamini na mfadhili wa Klabu yetu, Ghalib Said Mohammed (GSM), nipende kuwataarifu Wanachama na Mashabiki wa Klabu yetu kuwa leo, GSM ameridhia kwa dhati kushiriki kwenye kufanikisha ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Young Africans Sports Club, katika eneo la Makao Makuu ya Klabu yetu, Jangwani, Jijini Dar Es Salaam.

Nichukue fursa hii kumshukuru sana GSM kwa dhamira hiyo inayokwenda kutimiza ndoto ya Uongozi wangu, Kamati ya Utendaji na Wanachama na Mashabiki wa Young Africans kwa kuwa na uwanja wetu.

Kwa niaba ya Uongozi, Wanachama na Mashabiki wa Young Africans SC, nipende kumuahidi GSM, kuwa tutampa ushirikiano wote utakaohitajika kuhakikisha tunafanikisha ujenzi wa uwanja wetu.

Mungu ibariki Young Africans Sports Club, Mungu Ibariki Tanzania. Daima Mbele Nyuma Mwiko.

Injinia HERSI SAID, Rais wa Young Africans Sports Club

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Tags: , , , , , , ,

Comments are closed.