MATOLA Akiri Ubingwa Simba ni ngumu
MATOLA Akiri Ubingwa Simba ni ngumu
MATOLA Akiri Ubingwa Simba ni ngumu, Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola, amesema kupoteza tena mbele ya Yanga kumezidi kufanya safari ya Ubingwa kuwa ngumu.
Akizungumza baada ya dakika 90 za mchezo wa Derby ya Dar Es Salaam ama Kariakoo Derby kumalizika, Matola amekiri kuwa wamepoteza nafasi ya ushindani kuwania ubingwa msimu huu, lakini haina maana kwamba ndio mwisho wa msimu kwani bado wana mechi nyingine zilizobaki.
“Tulianza bila Mshambuliaji, lakini mara baada ya kufungwa mabao mawili, tukamuingiza Mshambuliaji ambaye amefunga bao la kufutia machozi,” amesema na kuongeza;
“Mabadiliko ya mapema pia tuliyoyafanya yametugharimu kwa sababu Mchezaji aliyeingia kafanya makosa, wapinzani wakapata faida ya penalti kutokana na kosa alilolifanya ndani ya 18.”
Matola amesema walikuwa wanatambua jeraha alilokuwanalo, Henock Inonga na waliamini ataweza kumaliza dakika 90, lakini mambo yameenda tofauti, huku akiweka wazi kuwa, beki huyo kapata jeraha jipya.
Inonga alilazimika kufanyiwa mabadiliko dakika ya 12 na nafasi yake kuchukuliwa na Hussein Kazi ambaye muda mchache tangu kuingia kwake, akasababisha penalti iliyokwenda kufungwa na Stephanie Aziz Ki.
Katika hatua nyingine, Matola amezungumzia namna timu yao ilivyo na makosa katika eneo la Ushambuliaji sambamba na ulinzi ambapo wameruhusu mabao kwenye kila mchezo.
“Tatizo la Washambuliaji na Wachezaji wanaopewa nafasi ya kucheza wamekuwa wakishindwa kutumia nafasi sawa na Mabeki makosa yamekuwa yakijirudia na sisi hilo tumeliona tutaenda kulifanyia kazi,” alisema Matola.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania April 03-2024
- USAJILI wa Watahiniwa wa Kujitegemea CSEE NA FTNA 2024
- RITA Uhakiki wa Vyeti vya Kuzaliwa na Vifo
- JINSI ya Kuangalia Majibu ya Uhakiki RITA
- RITA Utaratibu na Muongozo wa Kuhakiki Vyeti HESLB
- RITA Uhakiki wa Online System 2023/2024
- FAHAMU Kitambulisho Chako Cha NIDA Kilipo
- JINSI ya Kupata Police Loss Report Online
- AINA za Madaraja ya Leseni za Udereva
- JINSI ya Kupata Leseni ya Biashara Online
- JINSI ya Kupata TIN Number Online
- JINSI ya Kulipia Vifurushi vya Azam TV
- OUT yakaribisha maombi ya Udahili Muhula wa Kwanza 2023/2024
- MO Dewji Tajiri namba 12 Barani Africa 2024
- FOMU ya Maombi ya Kujiunga na VETA Tanzania 2024
- ORODHA ya Vyuo vya Ualimu Tanzania
- MFUMO wa Maombi ya Ajira Za Walimu OTEAS 2024/2025
- MSIMAMO NBC Championship 2023/2024
- Haya hapa Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- SHULE 10 Bora Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- MATOKEO Ya Darasa la Nne 2023/2024
- MATOKEO ya Kidato Cha Pili 2023/2024
- JINSI ya Kuangalia Matokeo Kidato Cha Nne 2023/2024
- ADA za Lipa kwa Airtel Mitandao Yote
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024
- TETESI Za Usajili Yanga SC Dirisha Dogo 2023/2024
- Ada/makato ya Lipa kwa M-pesa, Lipa kwa Simu
- ORODHA ya Vilabu Bora Afrika November 2023 (IFFHS Club Ranking)
- MSIMAMO Kundi D CAF Champions League 2023/2024
- MSIMAMO Wa Kundi B CAF Champions League Standings 2023/2024
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- MSIMAMO NBC Premier League 2023/2024
- WAFUNGAJI Wanaoongoza Magoli NBC Premier League 2023/2024
- KIKOSI cha Yanga SC msimu wa 2023/2024
- RATIBA Kamili Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Simba SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Yanga SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya England (EPL 2023/2024)
- KIKOSI cha Simba SC msimu wa 2023/2024